Maji safi na maji taka vyote ni changamoto Nairobi Kenya
Pakua
Uondoaji wa maji taka na upatikanaji wa maji safi ya kunywa vyote ni changamoto kubwa ambayo inakumba sehemu nyinyi na hasa miji ya nchi za Afrika. Kila mara mabomba ya maji taka hupasuka na kuvuja ambapo na ukarabati wa miundo mbinu muhimu kama hiyo huchukua muda mrefu na wakati mwingine kutelekezwa kabisa. Mji wa Nairobi nchini Kenya ni miongoni mwa miji inayokubwa na changamoto hizo mbili ambazo lengo namba la maendeleo endelevu namba 6 la Umoja wa Mataifa linasisitiza ni muhimu kwa kila mtu na kwa ajili ya maendeleo endelevu. je kwa sasa uko katika hali gani katika suala la huduma za maji taka na maji safi ya kutumika majumbani . Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi amefuatilia na kuandaa makala hii.
Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Jason Nyakundi
Audio Duration
4'32"