Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukikusanya chupa kulinda mazingira utazawadiwa:Inuka Foundation

Ukikusanya chupa kulinda mazingira utazawadiwa:Inuka Foundation

Pakua

Chupa na hasa la plastiki imekuwa moja ya tatizo kubwa la uchafuzi wa mazingira duniani na juhudi zinafanyika katika ngazi mbalimbali kuhakikisha taka hizo haziendeleo kuzagaa au kuishia baharini. Umoja wa Mataifa na wadau wako msitari wa mbele kuzichagiza jamii kuja na mbinu ya kupunguza taka hizo ikiwa ni pamoja na zile za kuzirejea na kutengeneza vitu vingine. Shirika la Inuka Foundation lililo na ofisi zake mjini Nairobi ni miongoni mwa wanaharakati hao wa mazingira  waliojitwika jukumu la kuhakikisha utunzi wa mazingira na hasa ukusanyaji wa taka za plastiki. Kwa kushirikiana na kampuni zinazotumia plastiki kama chupa, linatumia  teknolojia ya kuwazawadia pointi wanafunzi hasa wa vyuo vikuu wanapotumia chupa na kuziweka katika ndoo maalum ya kuzikusanya balada ya kuzitupa hovyo pointi ambazo huwanufaisha baadaye. Faith Chelangat ni mkuu wa programu katika shirika la Inuka Foundation amezungumza na mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi kuhusu mradi wao. 

Sauti
4'
Photo Credit
Picha ya UN /Martine Perret