Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pombe zilizoongezwa nguvu Bukavu zachochea ukatili wa kingono jimboni Kivu Kusini

Pombe zilizoongezwa nguvu Bukavu zachochea ukatili wa kingono jimboni Kivu Kusini

Pakua

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC,  vitendo vya ukatili wa kingono hususan ukatili majumbani huko DRC ukitambulika kama ujeuri wa kijinsia vimekuwa mwiba kwa maendeleo ya jamii,hususan wanawake, wasichana na watoto. Watoto wanakimbia nyumbani, wanawake wanatoa mimba na moja ya sababu ni wanaume kunywa pombe zilizoongezwa nguvu zaidi na hatimaye kupiga familia zao. Ni kwa kuzingatia hali hiyo ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO uliendesha mafunzo ya siku moja huko Bukavu jimboni Kivu Kusini kusaidia kuelimisha kuhusu ukatili wa kijinsia wakati wa siku 16 za kupinga  ukatili dhidi ya wanawake. Mafunzo hayo yaliendeshwa na kitengo cha jinsia cha Monusco kama anavyosimulia Brenda Mbaitsa kwenye makala hii.

Audio Credit
UN News/Brenda Mbaitsa
Audio Duration
3'40"
Photo Credit
UN Women