Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala ya Wiki

Unsplash/Drew Willson

Ni lazima wanawake tujiamini – Fundi viatu Jovia Kyomuhendo

Ubunifu ni moja ya mambo yanayotazamwa kuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Nchini Uganda, msichana Jovia Kyomuhendo amepata sifa kwa kuwa kijana mbunifu ambaye amefikia hatua ya kujiajiri kwa kuanzisha kiwanda kidogo cha kushona na pia kutengeneza viatu.

Safari yake imekuwaje hadi kufikia kutunukiwa tuzo na Muungano wa Viwanda Vidovidogo nchini Uganda USSIA? Tupate taarifa zaidi kutoka kwa mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego.

Sauti
3'41"
UN News/Devotha Songorwa

COVID-19 imekuwa mwiba kwa wavuvi mkoani Kigoma Tanzania

Janga la corona au COVID-19 limeendelea kuitikisa dunia kijamii na kiuchumi karibu kila pembe ya ulimwengu. Na hali ndivyo ilivyo kwa wavuvi wa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma ambako Devotha Songorwa kutoka Radio washirika TanzaniakidsTime FM amezungumza na wavuvi mbalimbali wa ziwa Tanganyika mkoani huo kutaka kujua je wanafahamu nini kuhusu janga hili , limewathiri vipi, na endapo wanatambua kuhusu suala la chanjo  na umuhimu wake katika kuwanusuru wavuvi na sekta hiyo wakati huu wa janga la COVID-19? Ungana nao katika Makala hii.

 

Sauti
5'37"
UNAMA/Eric Kanalstein

Mradi wa Mfereji wa Maji waboresha maisha ya wakazi wa Kabul, Afghanistan

Kila siku wananchi watano katika kijiji cha Pazhaki jimboni Kabul nchini Afghanisan walikuwa wanajukumu la kufungulia maji katika mfereji uliokuwa unategemewa na wanakijiji hao kwa shughuli za kilimo. Lakini Ramazan Ibrahimkil, mwenyekiti wa Kijiji cha Pazhak anasema alikuwa anapokea kesi kila uchwao kwamba wananchi wanaokaa milimani wakilalamikiwa kufungulia maji kwa wingi na hivyo wale wa mabondeni kukosa maji ya kutosha kwenye kilimo chao na hivyo kupata mazao machache na kipato kidogo. 

Sauti
4'41"
FAO/Giulio Napolitano

Udongo una umuhimu mkubwa kwa binadamu

Kuelekea siku ya udongo duniani tunaangazia mradi wa Shirika la chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kupitia mradi wa pamoja wa Kigoma (KJP) wa mafunzo kwa wakazi wa Kigoma nchini Tanzania.

Kwa upande wake Elizabeth Mrema Katibu mtendaji wa sekretarieti ya mkataba wa kimataifa kuhusu masuala ya Bayonuai (CBD) anasisitiza umuhimu wa kutunza bayonuai ya udongo.

Sauti
6'16"
FIB/MONUSCO

Uwepo wa vikosi vya FIB, MONUSCO DRC vimeweka mazingira ya usalama kwa jamii

Leo tunamulika ni kwa jinsi gani uwepo wa kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO umekuwa ni nuru kwa vijana na wafanyabiashara wa eneo la jimbo la Kivu Kaskazini. Shuhuda wetu huko si mwingine bali Luteni Issa Mwakalambo, afisa habai wa kikosi cha Saba cha Tanzania, 

Sauti
6'2"
UNICEF/Dejongh

Hali ya haki za watoto hususan Afrika Mashariki

Leo ni siku ya watoto duniani ikimulika kile ambacho kila mtu anafanya kuhakikisha kuwa dunia ni salama kwa mtoto wakati huu wa janga    la ugonjwa wa Corona au COVID-19. Umoja wa Mataifa una hofu kuwa janga hili linaweza kutowesha uzingatiaji wa misingi mikuu minne ya haki za mtoto ambayo ni kuishi, kuendelezwa, kushirikishwa na kulindwa. Je nini kinafanyika mashinani? Watoto wenyewe wanasemaje?

Sauti
7'53"