Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni lazima wanawake tujiamini – Fundi viatu Jovia Kyomuhendo

Ni lazima wanawake tujiamini – Fundi viatu Jovia Kyomuhendo

Pakua

Ubunifu ni moja ya mambo yanayotazamwa kuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Nchini Uganda, msichana Jovia Kyomuhendo amepata sifa kwa kuwa kijana mbunifu ambaye amefikia hatua ya kujiajiri kwa kuanzisha kiwanda kidogo cha kushona na pia kutengeneza viatu.

Safari yake imekuwaje hadi kufikia kutunukiwa tuzo na Muungano wa Viwanda Vidovidogo nchini Uganda USSIA? Tupate taarifa zaidi kutoka kwa mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego.

Jovia Kyomuhendo akieleza hisia zake baada kushinda tuzo ya kijana mbunifu mwaka jana anasema, “Eee! Mungu wangu, sikuamini kwamba ndio mimi aliyetuzwa kwa sababu tulikuwa na ushindani mkali uliohusisha wavulana na wasichana ambapo kila mmoja alikuwa anafahamu anachofanya.”

Tuzo hiyo iliadaliwa kijiimarisha katika utengenezaji wa vyatu ambapo kwa sasa anajiajiri mjini Kinubi, "lakini kwa nguvu za Mwenyezi mungu, nifanikiwa  kuwa wa pili. Nadhani hii ni kwa sababu nilikuwa najiamini sana kuhusu kile ninacchofanya. Na pia ninachofanya kinachangia kwneye uhifadhi wa mazingira kwani natumia magurudumu kutengeneza viatu hivyo na kuyaondoa katika mazingira.”

Wengi hushangaa wanapoona mwanamke akijishughulisha na utengenezaji wa viatu, “kila mtu huwa anasema ‘Eee” hiyo kazi ni ya wanaume lakini motisha ulionayo ndio inakusaidia kuchapa kazi. Je, unapenda kazi hiyo? Ikiwa unaipenda bila shaka unaweza kuifanya.”

Mazingira ya nyumbani hayakumruhusu Kyomuhendo kuendelea na elimu hadi elimu ya sekondari ya juu na vyuo. Lakini je, anajuta? “sijuti hata kidogo kwa sababu nimefanikiwa. Unakuta kwamba wengi wa walioendelea hadi kwneye vyuo vikuu hawana kazi lakini kwangu ninachapa kazi. Hata wakati wa COVID-19 nilikuwa nikifanya kazi kwani watu walikuwa wakitembea wakitumia viatu nikitengeneza na kuwashonea viatu vipya.”

Ujuzi huu umekuwa nuru kwa Kyomuhendo, kijamii na kiuchumi, “nimepata marafiki wengi sana na mawasiliano muhimu sana  duniani. Mfano ni USSIA ambao kupitia kwao nimepata tuzo. Tuzo ya kijana mbunifu”

Kwa upande wa kipato, “kiuchumi ninasema kwamba ninajitegemea. Sitegemei yeyote kwa sababu unakuta kwamba wasichana wengi hupenda kutegemea wengine kuwapatia mahitaji wakati wote, wakisema sisi wanawake ni wa kupewa na anakaa nyumbani lakini mimi ninajitegemea”

Kyomuhendo anaelezea kwa nini anapenda kazi yake hii, “kwa sababu nina soko kubwa sana kiasi kwamba kila mtu huvaa viatu. Wanawake, watoto wadogo, vijana na wazee hata babu yangu anavaa viatu. Inamaanisha hili ni soko kubwa sana lilopo”

Kwa mantiki hiyo, anatoa mawaidha kw awanawake, “ni kwamba sisi wanawake, ni lazima tujiamini. Kuwa mwanamke haimanishi kwamba hauwezi kufanya lolote. Usikubali kupuuzwa kwa sababu unaona sasa hivi mimi aliye mkode namna hivi ndio anayetengeneza viatu hivi”
Katika panda shuka ya maisha, Kyomuhendo amewahi kuwa mwalimu katika shule ya msingi na kuanza kuusomea ili awe mtaalamu lakini, aliaacha kwani alipata pesa za kununua machine alizokuwa anaihitaji ili ajiajiri katika utengenezaji wa viatu.

Audio Credit
John Kibego
Sauti
3'41"
Photo Credit
Unsplash/Drew Willson