Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala ya Wiki

Photo: WHO/A. Esiebo

Mchango wa wakunga wa jadi ni dhahiri hususan, Mwanza-Tanzania

Katika mfululizo wa makala zetu tukiangazia wakunga na wauguzi mwezi wa Februari, Leo tunaelekea mkoani Mwanza nchini Tanzania ambapo redio washirika, Redio SAUT, iliyoko mkoani Mwanza nchini Tanzania, katika makala iliyoandaliwa na Evarist Mapesa na kusimuliwa na Nyota Simba, inaangazia mkunga wa jadi Emmy Paulo Chalamila wa zahanati ya Igogo ya jijini Mwanza, Tanzania.

Sauti
5'27"
UN News/Grece Kaneiya

Meja Owuor, mwanamke wa shoka, mlinda amani kutoka Kenya

Moja ya vipaumbele vya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni kuhakikisha wanawake zaidi wanashiriki katika ulinzi wa amani hii ikiwa ni kutokana na hali ya sasa ambapo uwakilishi wa wanawake bado ni mdogo. Katika makala hii Flora Nducha wa UN News anazungumza na mwanamke wa shoka, mlinda amani kutoka Kenya na mmoja kati ya wanawake maafisa mafunzo ya kijeshi na peke yake kutoka Afrika Mashariki. Meja Veronica Owuor kabla ya kuja makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New york alikuwa afisa wa jeshi la anga la Kenya. Flora amemuuliza endapo kuna wanawake wengine katika wadhifa kama wake

Sauti
5'48"
Picha na UNCTAD/Adam Kane

Asasi ya kiraia yasaidia wanawake wanavikundi Geita Tanzania

Katika kufanikisha ustawi wa wanawake katika jamii, watu binafsi ikiwemo wanawake wenyewe wanajizatiti kujiimarisha kimaisha huku wakipata msaada kwa kuungana katika vikundi. Adelina Ukugani wa redio washirika Storm FM Geita amezungumza na wanawake wana vikundi ambao wanapata ushauri na usaidizi kutoka kwenye asasi ya kiraia ya Women’s Promotion Centre (WPC) huko Mgusu mkoani Geita nchini Tanzania.

Sauti
5'7"
FAO

Mabadiliko ya tabianchi yanaathiri mazao ya asili

Wakati wa maadhimisho  ya chakula duniani tarehe 16 mwezi huu wa Oktoba, suala la lishe bora liliangaziwa na zaidi ya yote nafasi ya vyakula asili. Hata hivyo mabadiliko ya tabianchi yameleta tafrashi katika baadhi ya maeneo ikiwemo Kagera nchini  Tanzania ambako mazao ya asili yametoweka. Je hali iko vipi? Ungana  basi na Nicolaus Ngaiza wa radio washirika Kasibante FM kwa ufafanuzi zaidi.

 

Sauti
8'31"
UN News/Grece Kaneiya

Elimu ni sehemu ya maendeleo na bila mwalimu hakuna elimu-Mwalimu Tabichi

Leo katika mada kwa kina tunaangazia siku ya walimu duniani ambayo huadhimishwa Oktoba 5 kila mwaka, mwaka huu kaulimbiu ikiwa ni “walimu vijana, mustakbali wa tasnia hii.” Lengo la siku ya walimu ikiwa ni kuwaenzi walimu kote ulimwenguni, kupongeza mafanikio na kuangalia changamoto zilizopo  kwa ajili ya kuimarisha tasnia hiyo. Mgeni wa siku ya leo kwa sasa anashikilia tuzo ya mwalimu bora kimataifa, tuzo ambayo ametunukiwa mapema mwaka huu kufuatia kujitolea kwake katika kazi ualimu.

Sauti
5'57"
UNnewskiswahili/Patrick Newman

Baada ya kunusurika kifo niliamua kuanzisha taasisi ya kusaidia wajane na mayatima-Bi Kamande

Dianah Kamande ni mama wa watoto wawili nchini Kenya ambaye katika mazingira ya kushangaza, siku moja mume wake alirejea nyumbani akiwa na nia moja tu, kumuua mkewe, wanaye wawili na kisha yeye mwenyewe ajiue. Ingawa watoto walitoroshwa haraka, mama yao hakuwa na bahati hiyo kwani alikatwakatwa kwa mapanga kichwani na sehemu nyingi za mwili hivi sasa zimepandikizwa vyuma na mishipa ya bandia.

Baada ya tukio hilo Dianah amebakia kuwa mjane kwani mume wake alijiua baada ya kufikiri kuwa ameshamuua mkewe.

Sauti
6'22"
© UNICEF/UN045727/Pirozzi

Usafirishaji haramu na changamoto zake Afrika Mashariki

Mapema wiki hii dunia imeadhimisha siku ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu huku Umoja wa Mataifa ukiutaja kama uhalifu mkubwa unaoshuhudiwa katika kila pembe ya dunia. Vita, mabadiliko ya tabicnhi,

umasikini na ubaguzi ni baadhi ya vitu ambavyo vimetajwa kuchochea wasafirishaji haramu kutumia fursa hizo kuendeleza biashara zao za kihalifu. Umoja wa Mataifa unahimiza kwamba juhudi za pamoja ni muhimu katika kusaidia kukomesha uhalifu huo na kuwaadhibu wahusika.Je nchi zinapambana vipi na uhalifu huo? namkaribisha Grace Kaneiya kwa maelezo zaidi

Sauti
5'48"
UN News/Video capture

Licha ya kupungua kwa mashambulio dhidi ya watu wenye ualbino, wanaishi kwa mashaka na hofu

Ingawa vitendo vya watu wenye nia ya uovu wa kuwashambulia watu wenye ualbino kuonekana kupungua, bado watu wenye ualbino wanaishi kwa mashaka na hofu kutokana na madhila wanayopitia katika maisha yao ya kila siku.

Kwa mtoto Mwigulu Matonange Magesa mwenye umri wa miaka 16 kutoka Tanzania kwa sasa, vitendo hivyo vimemsababishia kupoteza mkono wake mmoja katika kisa hiki anachosimulia alipohojiwa na Priscilla Lecomte kandoni mwa mkutano wa kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya watu wenye Ulemavu uliofanyika mjini New York Marekani. Ambatana nao katika makala ifuatayo.

Sauti
5'30"