Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala ya Wiki

FAO/Giulio Napolitano

Udongo una umuhimu mkubwa kwa binadamu

Kuelekea siku ya udongo duniani tunaangazia mradi wa Shirika la chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kupitia mradi wa pamoja wa Kigoma (KJP) wa mafunzo kwa wakazi wa Kigoma nchini Tanzania.

Kwa upande wake Elizabeth Mrema Katibu mtendaji wa sekretarieti ya mkataba wa kimataifa kuhusu masuala ya Bayonuai (CBD) anasisitiza umuhimu wa kutunza bayonuai ya udongo.

Sauti
6'16"
FIB/MONUSCO

Uwepo wa vikosi vya FIB, MONUSCO DRC vimeweka mazingira ya usalama kwa jamii

Leo tunamulika ni kwa jinsi gani uwepo wa kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO umekuwa ni nuru kwa vijana na wafanyabiashara wa eneo la jimbo la Kivu Kaskazini. Shuhuda wetu huko si mwingine bali Luteni Issa Mwakalambo, afisa habai wa kikosi cha Saba cha Tanzania, 

Sauti
6'2"
UNICEF/Dejongh

Hali ya haki za watoto hususan Afrika Mashariki

Leo ni siku ya watoto duniani ikimulika kile ambacho kila mtu anafanya kuhakikisha kuwa dunia ni salama kwa mtoto wakati huu wa janga    la ugonjwa wa Corona au COVID-19. Umoja wa Mataifa una hofu kuwa janga hili linaweza kutowesha uzingatiaji wa misingi mikuu minne ya haki za mtoto ambayo ni kuishi, kuendelezwa, kushirikishwa na kulindwa. Je nini kinafanyika mashinani? Watoto wenyewe wanasemaje? Basi tumulike hali Afrika Mashariki.

Sauti
7'53"
UN News/ John Kibego

Changamoto zitokanazo na ugonjwa wa kisukari

Tukielekea siku ya kisukari duniani hapo kesho shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linasema idadi ya wagonjwa wa kisukari duniani inaongezeka na ugonjwa huo unakatili maisha ya watu…. Kila mwaka. Ndio maana mwaka huu kaulimbiu ni waauguzi na kisukari ikiwa ni kampeni ya kuelimisha kuhusu umuhimu wa jukumu la watu hao katika vita dhidi ya kisukari.  Hata hivyo unapokuwa mkimbizi katika mkambini au makazi ya wakimbizi ukitegemea msaada kuweza kuishi kisukari ni msumari wa moto juu ya kidonda.

Sauti
7'12"
Video screenshot/Loise Wairimu

Kutoka Kenya hadi Marekani kupata mafunzo kwa vitendo

Loise Wairimu, ni msichana ambaye alifunga safari kutoka Kenya kuja hapa jijini New York Marekani katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ili apate mafunzo kwa vitendo.

Kwa takribani kipindi cha miezi sita amefanya kazi pamoja na timu nzima ya Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akichota maarifa ya kazi. Loise anaanza kwa kueleza namna safari yake hii ilivyoanza na alichojifunza mchakato huu.

Sauti
6'4"
UN / Anton Uspensky

Umoja wa Mataifa ukitimiza miaka 75 na mafanikio iliyoyafikia

Kesho ni siku ya Umoja wa Mataifa, chombo hicho kikitimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake! Katika mada kwa kina Anold Kayanda anatupitisha safari ya kuanzishwa kwake na zaidi ya yote simulizi ya mtu aliyezaliwa mwaka mmoja na Umoja wa Mataifa, mtu ambaye amewahi kushika nyadhifa ndani ya Umoja wa Mataifa, barani Afrika na ndani ya taifa lake la Tanzania. Kwako Anold!

Sauti
5'24"
WHO/P. Virot

Watu bilioni 1 duniani wanaishi na matatizo ya akili-Takwimu

Kuelekea siku ya afya ya akili duniani itakayoadhimishwa kesho Jumamosi Oktoba 10, takwimu zinaonesha kuwa takribani watu bilioni 1 duniani kote wanaishi na matatizo ya akili. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kwa siku hii amesema, inabidi hatua zichukuliwe ili kuhakikisha kunakuwa na huduma bora ya afya ya akili kwa wote kwani hivi sasa inaonesha pia kuwa kila sekunde 30 mtu mmoja anajiua kutokana na tatizo hili la afya ya akili. 

Sauti
5'42"