Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala ya Wiki

26 Julai 2019

Jaridani Julai 26, 2019 na Arnold Kayanda- ikiwa ni Ijumma

Habari kwa Ufupi kuanzia Homa ya ini, mashambulizi ya anga Syria na Hatua dhidi ya kukabiliana na Ebola.

Katika mada kwa kina tunasikia kutoka kwa kijana Mwiguli ambaye anaulabino akisimulia alivyonusurika kifo huku akikatwa mkono.

Na kwenye Neno la Wiki linachambuliwa neno Afkani.

Sauti
9'54"
Smart Kaya

Akili bandia na matumizi yake nchini Tanzania

Akili Bandia hivi sasa imeanza kushika kasi na pengine ni wengi wetu bado kufahamu teknolojia hii ambayo tayari imebisha hodi pale tulipo. Kufahamu kwa kina ina maana gani Assumpta Massoi amezungumza na Castory Munishi, mwanafunzi katika Chuo KIkuu cha sayansi za tiba Muhimbili au MUHAS nchini Tanzania ambao hivi karibuni walikuwa na mdahalo kuhusu akili bandia na nafasi yake katika huduma za afya. Bwana Munishi anaanza kwa kuainisha neno akili bandia.

 

Sauti
6'19"
UN News/Yasmina Guerda

Matumizi ya tumbaku na athari zake

Maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya kupinga matumizi ya tumbaku yanataka kila mtu kuepusha moshi wa sigara ambapo shirika la afya ulimwenguni, WHO limekuja na maudhui, usikubali tumbaku  ichukue pumzi yako. Kwa mantiki ya kwanza waangazia madhara ya moshi wa sigara kwenye mapafu na kadhalika. Makala imejikita katika uraibu wa matumizi ya tumbaku na madhara yake huku wachangaiji wa leo wakiwa nchini Tanzania ambapo Patrick Newman ametuandalia makala ifautayo 

Sauti
5'1"
©FAO/Christabel Clark

Hatua dhidi ya athari ya mabadiliko ya tabianchi Kenya

Dunia imeadhimisha siku ya familia Mei 15, mwaka huu ikibeba kaulimbiu familia na hatua katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Hatua hii ni kufuatia mabadiliko ya tabiachi yanayoshuhudiwa duniani kote huku athari zake zikiwakumba watu wote.  Grace Kaneiya amezungumza na familia moja huko nchini Kenya ambao wanashiriki kilimo lakini pia ni wafugaji huku wakichukua hatua kulinda mazingira, Je wamechukua hatua zipi? Basi sikiliza makal ifuatayo kwa undani zaidi. 

Sauti
5'26"
UNnewskiswahili/Patrick Newman

Suala la jinsia linaibuka hata katika kupanda cheo cha uaskofu- Mchungaji

Uongozi katika jamii nyingi ni nafasi ambayo kwa mtazamo wa wengi ni ya wanaume na ndio maana lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka fursa sawa za uongozi kwa wote, wake kwa waume, bila ubaguzi wa aina yoyote ile. Hali hiyo ya mkwamo inamkabili pia mchungaji mwanamke Dkt. Lydia Mwaniki kutoka Kenya ambaye licha ya kuwa mchungaji, suala la kupanda cheo cha uaskofu linakabiliwa na changamoto ya jinsia yake.

Sauti
3'31"
UN News Kiswahili

Kiswahili chazidi kupasua mawimbi ya bahari na mawingu hata ughaibuni

Kiswahili! Kiswahili! Kiswahili! Kinazidi kupasua mawimbi ya bahari na mawingu na kuwa kivutio siyo tu kwa watu wazima bali pia watoto wadogo tena ughaibuni.

Huyu ni Braydon Bent, mchambuzi wa soka pengine mdogo zaidi barani Ulaya akijinasibu kwa lugha ya Kiswahili na kuleta msisimko mkubwa kwa mashabiki wake. Mwenzangu Arnold Kayanda amezungumza na mwalimu wa Kiswahil wa Braydon aitwae John Jackson hivi sasa mkazi wa Ujerumani akianza kwanza kwa kuelezea kilichomvutia na Kiswahili.

Sauti
5'43"
UNICEF/Christine Nesbitt

Wakazi wa Geita na Kagera nchini Tanzania 'wafunguka' kuhusu huduma za bima ya afya

Serikali za nchi mbalimbali kote duniani ziko katika mchakato wa kuhakikisha zinawawezesha wananchi wao kuwa na bima ya afya ambayo inawaruhusu kupata huduma ya afya wakati wowote, popote na kwa kila mtu. Juhudi hizi ni katika kutekeleza malengo yaliyowekwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuwa ifikapo mwaka 2030 kila mtu bila kujali hali yake awe na uwezo wa kupata huduma ya afya. Je! Baadhi ya wananchi wa Tanzania wanasemaje kuhusu Bima ya afya? Tuanzie mkoani Geita kwake Adelina Ukugani wa redio washirika, Storm FM.

Sauti
5'14"
Shutterstock

Chuo cha BareFoot chaleta mabadiliko kwa wanawake Zanzibar

Leo katika makala yetu Flora nducha wa Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na Pendo Yeredi Daudi Mratibu wa chuo cha Bearfoot kilichoanziswa na serikali ili kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanawake wa vijijini huko visiwani Zanzibar, mafunzo ambayo yamekuwa mkombozi mkubwa kwao. Miongoni mwa mafunzo hayo ni ya mradi wa kutengezeza paneli za nishati ya jua au sola. Mradi huo unaendeshwa na wanawake tu tena wa vijijini maarufu kama sola mamamazi , umeleta tija kwa wanawake hao, familia zao na jamii kwa ujumla.

Sauti
5'49"
UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya

Mchango wa wanawake katika kuchagiza amani Kenya

Mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW63 unafunga pazia leo Machi 22 hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Mkutano huu ambao umewaleta pamoja zaidi ya washiriki 9000 kutoka wawakilishi wa nchi 193 wanachama wa umoja huo pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale ya kiraia umejadili  jinsi gani mwanamke ataweza kukombolewa katika suala zima la uongozi lakini vilevile kumpatia mwanamke uwezo wa kuongeza mchango wake katika jamii.

Sauti
5'54"