Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala ya Wiki

UN News/Yasmina Guerda

Viongozi wakifahamu kuhusu mabadiliko ya tabianchi, kazi inakuwa rahisi: UNEP

Mkutano wa 24 wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (COP24) umekamilika huko mjini Katowice Poland. Baada ya wiki mbili za majadiliano ya makundi zaidi ya 200 yameidhinisha muongozo wa utekelezaji wa mkataba wa Paris wa mwaka 2015, wenye lengo lakupunugza ongezeko la joto duniani kuwa chini ya nyuzi joto 2.

Mkutano huo umeeleza kuwa ingawa kuna hatua ambazo zimepigwa, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kufikia makubaliano ya mkataba wa Paris hasa kwa nchi zinazoendelea.

Sauti
2'41"
UN News/Patrick Newman

Siamini mimi leo nimeingia jengo la UN New York- Judith

Vijana ndio nguzo ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Ni kwa kuzingatia hilo, katika kila vikao vinavyofanyika vya Umoja wa Mataifa kuhusu SDGs, vijana wanashirikishwa ipasavyo ili kujumuisha sauti zao kutoka mashinani. Hata hivyo baadhi ya vijana wamekuwa wakisitasita kushiriki katika kufanikisha malengo yao, iwe kwa kufahamu au kutofahamu na hivyo kusalia nyuma.

Sauti
4'

Katika SDGs tunasonga na UN imetia shime- Balozi Mushi

Nchini Tanzania, Umoja wa Mataifa uko bega kwa bega na serikali kufanikisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yaliyopitishwa mwaka 2015. Takribani miaka mitatu imepita tangu kupitishwa na ukomo ni mwaka 2030. Malengo yako 17 na kila nchi inajipigia upatu kuwa inasonga mbele kufanikisha malengo hayo kuanzia kutokomeza umaskini hadi kujenga ubia wa kimataifa. Je Tanzania pamoja na Umoja wa MAtaifa kutia shime, serikali yenyewe inafanya nini? AssumptaMassoi amezungumza na Mkurugenzi wa uhusiano wa kimataifa katika wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo, Balozi Celestine Mushi.

Sauti
4'3"
Mwanza Youth reporter

Wasichana shirikini michezo kwa kucheza na kutangaza

Radio, michezo na jinsia ni mada ambayo imechambuliwa kwa kina na vijana wa mtandao wa wanahabari vijana kutoka Mwanza nchini Tanzania. Uchambuzi huo umeendana na maudhui ya siku ya redio duniani hii leo ya Radio na Michezo. Katika makala hii, mwanahabari kijana Rashid Malekela anazungumza na vijana wenzake wa kike na wa kiume kufahamu ni kwa jinsi gani mada hizo zinaoana na zaidi ya hapo zinasaidiaje kubeba jukumu kubwa la radio la kuliemisha, kuhabarisha na kuburudisha.

Sauti
4'5"