Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanamke, kwenye uongozi huletewi kadi kama harusi - Balozi Getrude Mongela

Mwanamke, kwenye uongozi huletewi kadi kama harusi - Balozi Getrude Mongela

Pakua

Kikao hiki cha 65 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani kilichoanza tarehe 15 Machi kikiwa sasa kinakamilisha wiki yake ya kwanza, wadau kwa namna mbalimbali kote duniani wanaendelea kujadili mada ya mwaka huu ambayo imejikita kwenye kuangazia wanawake katika uongozi ili kufikia dunia yenye usawa. 

Kupitia mahojiano haya yaliyofanywa na Stella Vuzo wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam, Tanzania, Balozi Getrude Mongela ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa mkutano wa kimataifa wa 4 wa wanawake uliofanyika Beijing, China miaka 25 iliyopita na ameshika nafasi mbalimbali za uongozi nchini mwake Tanzania na kwingineko kimataifa, je ana lipi katika suala hili la wanawake na uongozi? 

Audio Credit
Stella Vuzo/ Getrude Mongella
Audio Duration
6'42"
Photo Credit
UN Tanzania