Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

5 Aprili 2022

Jaridani na Leah Mushi-

Watoto 3 kati ya 10 hawamalizi elimu ya msingi Madagascar : UNICEF

Nusu ya wananchi wote Afghanistan hawana uhakika wa chakula : FAO

Buriani walinda amani 8 wa Umoja wa Mataifa nchini DRC

Makala tunasalia DRC 

Mashinani ni wito kwa jamii ya kimataifa kuhusu kutokatisha msaada kwa Somali wakati hali ya utulivu ikiimarika.

Sauti
12'2"

4 Aprili 2022

Jaridani Aprili 4, 2022 na Leah Mushi 

-Karibu watu wote duniani, asilimia 99 wanavuta hewa isiyo salama iliyopita viwango vya ubora wa hewa vilivyowekwa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na hivyo kutishia afya zao.

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antinio Guterres leo ameonya kwamba dunia inaelekea pabaya linapokuja suala la mabadiliko ya tabianchi ,na ni suala la aibu linaloambatana na ahadi hewa  zinazomuweka kila mtu kwenye hatari ya zahma kubwa.  

Sauti
11'28"

01 APRILI 2022

Kuelekea maadhimisho ya kuelimisha jamii kuhusu usonji tarehe 02 Aprili hii leo katika mada kwa kina tunakwenda nchini Kenya katika eneo la Roysambu jijini Nairobi, kwenye shule inayofundisha Watoto wenye usonji iitwayo, Kenya Community Center for Learning. 

Umoja Mataifa unataka ujumuishi wa Watoto wenye usonji ikiwa ni moja ya vipengele vya lengo namba 4 la malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs. Je nini kinafanyika huko, mwandishi wetu nchini Kenya, Thelma Mwadzaya ametuandalia mada hii kwa kina.

Sauti
11'22"

30 Machi 2022

Hii leo Jumatano katika Jarida tuna habari kwa ufupi zikimulika mimba zisizotarajiwa kuwa ni janga lilipouuzwa; misaada ya kibinadamu yafika eneo muhimu zaidi huko Ukraine ambako misaada ilikuwa haijafika tangu vita ianze mwezi uliopita na kisha miongozo mipya ya WHO ya kusaidia wanawake na watoto siku za mwanzo tu baada ya mtoto kuzaliwa. Mada kwa kina ni sehemu ya pili na ya mwisho ya mahojiano na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake , Wazee na Makundi Maalum, Dkt.

Sauti
12'1"

29 Machi 2022

Watoto 330,000 Somalia hatarini kufariki dunia kutokana na unyafuzi- UNSOM

WHO yatoa huduma za matibabu na usaidizi wa kisaikolojia kwa wakimbizi wa Ukraine

Msichana Manuela Christine kinara wa kuhamasisha wasichana kubaki katika shule Uganda

Makala ni mafunzo kuhusu ulinzi wa mazingira

Katika mashinani tutasikia kutoka kwa mkurugenzi mkuu mpya wa ILO.

Sauti
14'16"

28 Machi 2022

Jaridani Machi 28, 2022 na Leah Mushi tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumulika changamoto za maji kwenye makambi ya wakimbizi. Pia tutasikia habari kwa ufupi zikiangazia, silaha za vilipuzi, hali ya watoto nchini Syria na ukiukwaji wa haki nchini Libya.

Sauti
12'54"

25 MACHI 2022

Jaridani Machi 25, 2022 na Flora Nducha 

Tunaanza na habari kwa ufupi kisha mada kwa kina ambapo leo tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kukutana na mpiganaji wa zamani wa msitu ambaye sasa ameajiriwa na Umoja wa Mataifa. Na ikiwa IJumaa tutajifunza kiswahili

Sauti
15'24"

23 MACHI 2022

Katika Jarida la Jumatano Machi 23, 2022 kuna habari kwa ufupi zilkilenga mateso yanawowakibili wanawake wakati wa kujifungua, ujumbe wa Katibu Mkuu katika siku ya utabiri wa hali ya hewa duniani na wito wa ILO kwa Russia kukomesha uvamizi Ukraine pia  tunaangazia kikao cha 66 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani kinachoendelea hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa na hususan hatua zilizopigwa na Tanzania katika kusongesha usawa wa kijinsia, kwenye mashinani tutasikia kuhusu msaada linalotoa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Poland.

Sauti
12'39"