Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 Machi 2022

30 Machi 2022

Pakua

Hii leo Jumatano katika Jarida tuna habari kwa ufupi zikimulika mimba zisizotarajiwa kuwa ni janga lilipouuzwa; misaada ya kibinadamu yafika eneo muhimu zaidi huko Ukraine ambako misaada ilikuwa haijafika tangu vita ianze mwezi uliopita na kisha miongozo mipya ya WHO ya kusaidia wanawake na watoto siku za mwanzo tu baada ya mtoto kuzaliwa. Mada kwa kina ni sehemu ya pili na ya mwisho ya mahojiano na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake , Wazee na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima kutoka Tanzania akizungumza na Flora Nducha wakati akiwa hapa Marekani kushiriki mkutano wa 66 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW66. Leah Mushi anatamatisha jarida na mashinani na anasalia huko huko Tanzania wilayani Ngorongoro kumsikia mnufaika wa mradi wa Umoja wa Mataifa. Karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'1"