Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

01 APRILI 2022

01 APRILI 2022

Pakua

Kuelekea maadhimisho ya kuelimisha jamii kuhusu usonji tarehe 02 Aprili hii leo katika mada kwa kina tunakwenda nchini Kenya katika eneo la Roysambu jijini Nairobi, kwenye shule inayofundisha Watoto wenye usonji iitwayo, Kenya Community Center for Learning. 

Umoja Mataifa unataka ujumuishi wa Watoto wenye usonji ikiwa ni moja ya vipengele vya lengo namba 4 la malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs. Je nini kinafanyika huko, mwandishi wetu nchini Kenya, Thelma Mwadzaya ametuandalia mada hii kwa kina.

Na katika kujifunza Kiswahili tutaelekea Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA kwake Katibu Mtendaji Dkt. Mwanahija Ali Juma akifafanua maana ya methali Mnyamaa kadumbu! 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
11'22"