Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

4 Aprili 2022

4 Aprili 2022

Pakua

Jaridani Aprili 4, 2022 na Leah Mushi 

-Karibu watu wote duniani, asilimia 99 wanavuta hewa isiyo salama iliyopita viwango vya ubora wa hewa vilivyowekwa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na hivyo kutishia afya zao.

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antinio Guterres leo ameonya kwamba dunia inaelekea pabaya linapokuja suala la mabadiliko ya tabianchi ,na ni suala la aibu linaloambatana na ahadi hewa  zinazomuweka kila mtu kwenye hatari ya zahma kubwa.  

-Na leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu mabobu yaliyotegwa ardhini mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM umesema mabaki ya vilipuzi vya silaha za vita na mabomu ya kutegwa ardhini yameendelea kuleta athari kubwa kwa raia wa Somalia na hivyo umeahidi msaada wake kwa taifa hilo la Pembe ya afrika kuhakikisha linakuwa huru na mabomu hayo ya ardhjini na vilipuzi vingine.

Kwenye makala tunasikia kuhusu mzazi wa mtoto wenye usonji.

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
11'28"