Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

09 Machi 2022

Hii leo jaridani Leah Mushi anakutelea Habari kwa Ufupi zikisomwa na Flora Nducha ambamo anaangazia mwongozo wa WHO wa utoaji mimba ulio salama, madhila zaidi kwa wananchi wa Syria ambako mzozo unaingia mwaka wa 12 na UNICEF yapeleka dawa kunusuru wanawake na watoto majimbo ya Beni na Yobe nchini Nigeria.

Sauti
14'29"

08 Machi 2022

Hii leo jaridani ni siku ya wanawake tukimulika ujumbe kuanzia ngazi ya Umoja wa Mataifa wa kutaka ujumuishaji wa wanawake katika ngazi zote za maendeleo ili kufanikisha ajenda 2030 ya maendeleo endlevu. Huko Uganda wakimbizi na wenyeji kwenye makazi ya wakimbizi ya Kyangwali ni shamrashamra na ujumbe mahsusi wa siku ya leo ya wanawake duniani.

Sauti
13'59"

07 Machi 2022

Leo jaridani Leah Mushi anakuletea mada kwa kina ikiangazia siku ya wanawake duniani kesho Machi 8 ambapo kutoka Tanzania Mratibu wa shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP nchini humo anamulika umuhimu wa wanawake na mazingira katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Lakini kwanza ni habari kwa ufupi kuhusu mauaji ya walinda amani wanne wa Umoja wa Mataifa huko Mali; watoto wanaokimbia Ukraine bila wazazi na walezi na umuhimu wa kuwekeza katika sekta ya huduma na malezi kwa watoto, wazee na wagonjwa ili kuongeza ajira milioni 300 ifikapo mwaka 2035.

Sauti
10'31"

04 Februari 2022

Hii leo jaridani Leah Mushi ana mambo makuu matatu: 
1.    Muhtasari wa Habari ukimulika Ukraine hasa kupitishwa kwa azimio la kuanzisha Kamisheni ya kuchunguza madhila yatokanayo na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Kuanzishwa kwa njia ya kuwezesha raia kuondoka Ukraine na hatimaye Ethiopia ambako hali huko Tigray na Amhara yatia hofu licha ya kuimarika hivi karibuni.

Sauti
12'

3 Machi 2022

Jaridani hii leo Leah Mushi anaanzia huko Ukraine ambako mashambulizi yanayoaendelea yanahatarisha afya ya uzazi ya wanawake na watoto wa kike. Kisha anamulika siku  ya kimataifa ya wanyapori akiangazia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kutaka kuendelea kulindwa kwa wanyamapori kwa maslahi ya binadamu na sayari duniani. Suala la uwezeshaji wanawake kiuchumi linamulikwa pia kwa kubisha hodi Kigoma nchini Tanzania ambako Umoja wa Mataifa kupitia FAO unawapa wanawake uwezo wa kujiamini kupitia kilimo cha maharage.

Sauti
13'25"

02 MACHI 2022

Katika jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Leah Mushi anakuletea

-Idadi ya watu waliokimbia mashambulizi nchini Ukraine katika kipindi cha siku 6 zilizopita ni zaidi ya 870,000, limesema hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, kupitia jukwaa lake lililozindua ili kuonesha takwimu za watu wanaokimbia wakiwemo raia na wageni. 

Audio Duration
11'29"

01 Machi 2022

Karibu kusikiliza jarida ambapo miongoni mwa utakayosikia ni pamoja na ombi la fedha za kusaidia wakimbizi nchini Ukraine

Hali inavyoendelea nchini Madagascar baada ya kukumbwa na vimbunga vinne katika kipindi kifupi 

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa Tanzania kikosi cha TANZBAT-8 wametoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC

Na FAO imehimiza wavuvi wadogo wafdogo wasipuuzwe kwakuwa wanaumuhimu mkubwa hasa kwenye masuala ya lishe. 

Sauti
15'11"

28 Februari 2022

karibu kusikiliza jarida na kama ilivyo ada kila Jumatatu tunakuletea mada kwa kina, mahojiano maalumu na mmoja wa waliokuwa ngariba nchini Tanzania lakini sasa ameacha shughuli hiyo ya ukeketaji baada ya kuelimika.

Pia Flora Nducha atakuletea habari kwa ufupi kubwa likiwa ni mapigano nchini Ukraine na namna Umoja wa Mataifa unavyoshughulikia.

 

Sauti
14'53"

28 Februari 2022

karibu kusikiliza jarida na kama ilivyo ada kila Jumatatu tunakuletea mada kwa kina, mahojiano maalumu na mmoja wa waliokuwa ngariba nchini Tanzania lakini sasa ameacha shughuli hiyo ya ukeketaji baada ya kuelimika.

Pia Flora Nducha atakuletea habari kwa ufupi kubwa likiwa ni mapigano nchini Ukraine na namna Umoja wa Mataifa unavyoshughulikia.

 

Sauti
14'53"

25 FEBRUARI 2022

Karibu kusikiliza jarida ikiwa leo ni siku ya mada kwa kina kunaelekea nchini Uganda kuangazia kwa undani athari  za kiuchumi za mafuriko ambayo yamedumu kwa miaka miwili sasa kwa wakazi hasa wa ziwa Albert baada ya kusababisha hasara kubwa ya mali.

Pia utasikia habari kwa ufupi zikisomwa na Flora Nducha na kubwa ni kuhusu msaada wa kibinadamu kwa wananchi wa Ukraine pamoja na Madagascar. 

Sauti
12'58"