Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

21 Aprili 2022

Hii leo jaridani Grace Kaneiya anaanzia huko Ukraine ambako idadi ya wakimbizi wa ndani inazidi kuongezeka kutokana na vita vinavyoendelea. Kisha anakwenda Kenya kuona jinsi wafanyakazi wa kujitolea wa kijamii wameweza kushawishi wanajamii kukubali chanjo dhidi ya COVID-19. Atasalia huko huko Kenya ambako mashirika ya Umoja wa Mataifa yameleta nuru kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwapatia mradi wa umwagiliaji maji. Makala tunafunga safari hadi Brazili kuangazia maisha ya wahamiaji na wakimbizi ambao ni watu wa asili wa Warao kutoka Venezuela.

Sauti
13'18"

20 Aprili 2022

Hii leo jaridani na Grace Kaneiya ni mada kwa kina ikimulika harakati za taasisi ya TAI nchini Tanzania ya kutumia michezo ya kuigiza, vikaragosi, au katuni za kwenye majarida au zenye sauti kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo haki, elimu na afya. Anold Kayanda amezungumza na Ian Tarimo, kiongozi wa taasisi hiyo ambaye alikuwa jijini New York, Marekani.

Sauti
13'28"

19 Aprili 2022

Karibu jaridani hii leo na Grace Kaneiya akianzia Uganda ambako UNICEF na serikali ya Iceland wamefanikisha  mradi wa kuhakikisha huduma ya maji safi na kujisafi (WASH) kwa wanafunzi wote kwenye shule za wilaya za Adjumani na Arua nchini Uganda. Kisha anabisha hodi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC huko serikali imepatia wakimbizi na wenyeji ardhi ya ekari 500 kuimarisha kujitegemea, mkimbizi katoa shukrani. Jarida linasalia huko huko DRC kumulika juhudi za UNICEF kuona watoto wanasoma licha ya kuishi kwenye vituo vya ukimbizini.

Sauti
12'51"

18 Aprili 2022

Hii leo katika Jarida la Habari tunamulika kwa kina ukame na njaa Pembe ya Afrika ambapo Msadizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya dharura, OCHA. Bi. Joyce Msuya anazungumzia kile ambacho wanafanya kusaidia wakazi wa eneo hilo. Habari kwa Ufupi inamulika chanjo ya Polio Ethiopia, uzinduzi wa kituo cha kimataifa cha tiba asilia nchini India na kumalizika kwa mzozo baina ya jamii a walendu na wahema huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, waliokuwa wakizozozana juu ya matumizi ya kanisa.

Sauti
12'31"

14 Aprili 2022

Jaridani Aprili 14, 2022 na Leah Mushi

-Watu milioni 7 wameambukizwa chagas, upimaji na tib ani muhimu:WHO/UNITAID

-Tunazifuatilia taarifa kuwa Uingereza inataka kuwahamishia nchini Rwanda wasaka hifadhi

-Programu za mlo shuleni ni daraja la kufikia ndoto za elimu kwa watoto masikini :WFP

Sauti
11'34"

13 Aprili 2022

Jaridani na Leah Mushi kwanza ni habari kwa ufupi kisha katika mada kwa kina tunarejea makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa mahojiano maalum na waziri wa madini wa Tanzania kuhusu migogoro na rasilimali za madini ikiwemo almasi.

Mashinani ni athari za mgogoro wa Ukraine kwa uchumi wa nchi mbalimbai duniani.

Sauti
12'22"

12 Aprili 2022

Jaridani Jumanne, Aprili 12, 2022-

-Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameonya kuwa janga lingine la njaa kama la mwaka 2011 linanyemelea Somalia iwapo wahisani hawataongeza ufadhili wao kwa ombi la usaidizi wa kibinadamu kwa taifa hilo la pembe ya Afrika kwa kuwa ukame wa muda mrefu sambamba na ongezeko la bei za vyakula vimeongeza idadi ya wasio na uhakika wa chakula kufikia watu milioni 6, sawa na asilimia 40 ya wananchi wote.

Sauti
14'13"

11 Aprili 2022

Jaridani Aprili 11, 2022 na Leah Mushi

Kwanza ni Habari kwa ufupi-

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP limetangaza programu ya kusaidia mahitaji ya mamilioni ya watu nchini Ukraine katika kipindi cha miaka miwili ijayo. 

8 Aprili 2022

Katika Jarida la Ijumaa Aprili 8, 2022 na Leah Mushi ameeanza na habari muhimu kwa siku ikiwemo:

Takriban watu milioni 15 wameathriwa vibaya na ukame nchini Kenya, Somalia na Ethiopia likwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM. 

Shirika hilo limeongeza kuwa huu ni ukame mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa ukisababisha mamilioni ya watu kutawanywa, kutokuwa na uhakia wa chakula na kuharibu ardhi ya kilimo na mazao.  

Sauti
12'57"

07 Aprili 2022

Ungana na Leah Mushi anayekuletea jarida hii leo likianza na maadhimisho ya siku ya afya, WHO imetoa wito kwa serikali na wananchi kwa ujumla kutunza mazingira. 

Leo pia ni siku ya kumbukizi ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda dhidi ya watutsi ya mwaka 1994 hayakuwa ya bahati mbaya ya yalikuwa yanaweza kuzuilika. 

pia utasikia kuhusu walinda amani wa Tanzania waliotembelea wafungwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Makala kutoka Zambia kuhusu ardhi oevu na ujumbe kwa watu kuendesha baiskeli kwa ajili ya kulinda afya zao. 

Karibu usikilize. 

Sauti
12'28"