Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 Aprili 2022

14 Aprili 2022

Pakua

Jaridani Aprili 14, 2022 na Leah Mushi

-Watu milioni 7 wameambukizwa chagas, upimaji na tib ani muhimu:WHO/UNITAID

-Tunazifuatilia taarifa kuwa Uingereza inataka kuwahamishia nchini Rwanda wasaka hifadhi

-Programu za mlo shuleni ni daraja la kufikia ndoto za elimu kwa watoto masikini :WFP

Kwenye makala, tumsikilize muuguzi Rebecca Deng ambaye ni mkimbizi wa Sudani Kusini aliyeko katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya na kupitia programu ya Uzazi Salama inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR kwakushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya amekuwa akitoa elimu kwa jamii juu ya afya ya uzazi.

Mashinani tunakutana na afisa wa lishe wa UNICEF akiwa Oromia, Ethiopia.

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
11'34"