Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

8 Aprili 2022

8 Aprili 2022

Pakua

Katika Jarida la Ijumaa Aprili 8, 2022 na Leah Mushi ameeanza na habari muhimu kwa siku ikiwemo:

Takriban watu milioni 15 wameathriwa vibaya na ukame nchini Kenya, Somalia na Ethiopia likwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM

Shirika hilo limeongeza kuwa huu ni ukame mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa ukisababisha mamilioni ya watu kutawanywa, kutokuwa na uhakia wa chakula na kuharibu ardhi ya kilimo na mazao.  

Hivyo IOM imetoa wito wa hatua za haraka za kibinadamu ili kuepusha janga kubwa la kibinadamu katika ukanda huo wa Pembe ya Afrika.  

 

=================================================  

 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema vita nchini Ukraine vimesababisha moja ya ongezeko kubwa kabisa na la haraka la watu kutawanywa na janga la kibinadamu kuwahi kutokea.  

 Shirika hilo linasema ndani ya wiki sita pekee zaidi ya watu milioni 4.3 wamekimbia nchi yao na kuwa wakimbizi huku wngine milioni 7.1 wametawanywa ndani ya Ukraine.  

 UNHCR inashirikiana  kwa karibu na mamlaka ndani ya Ukraine ili kuongeza uwezo wa meneo yanayopokea wakimbizi. UNHCR pia inashirikiana na mamlaka katika maeneo mbalimbali kubainisha majengo yanayohitaji kufanyiwa ukarabati ili kutumika kama vituo vya mapokezi au vya kuwaleta  watu pamoja. 

 

Na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC sasa imejiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwa mwanachama wa saba. Rais wa DRC Tshisekedi aliye ziarani Kenya kwa siku mbili ametia rasmi saini mkataba wa uanachama. Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo ndiyo nchi kubwa zaidi kwenye eneo lililo kusini mwa jangwa la sahara Na ya pili barani Afrika. Jumuiya ya Afrika Mashariki iliasisiwa mwaka 1967 , ikasambaratika baada ya miaka kumi na kufufuliwa upya mwaka 2000.Pindi baada ya hafla hiyo iliyofanyika Ikulu ya Nairobi kukamilika katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dr Peter Mathuki alielezea manufaa ya DRC kuwa mwanachama. 

Mada kwa kina ni mazungumzo na balozi Gaston, mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa amezungumza na idhaa hii.

 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'57"