Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 Aprili 2022

21 Aprili 2022

Pakua

Hii leo jaridani Grace Kaneiya anaanzia huko Ukraine ambako idadi ya wakimbizi wa ndani inazidi kuongezeka kutokana na vita vinavyoendelea. Kisha anakwenda Kenya kuona jinsi wafanyakazi wa kujitolea wa kijamii wameweza kushawishi wanajamii kukubali chanjo dhidi ya coronavirus">COVID-19. Atasalia huko huko Kenya ambako mashirika ya Umoja wa Mataifa yameleta nuru kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwapatia mradi wa umwagiliaji maji. Makala tunafunga safari hadi Brazili kuangazia maisha ya wahamiaji na wakimbizi ambao ni watu wa asili wa Warao kutoka Venezuela. Tamati ya jarida la leo ni mashinani ikibisha hodi nchini Malawi. Karibu!

Audio Credit
Grace Kaneiya
Audio Duration
13'18"