Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 Aprili 2022

19 Aprili 2022

Pakua

Karibu jaridani hii leo na Grace Kaneiya akianzia Uganda ambako UNICEF na serikali ya Iceland wamefanikisha  mradi wa kuhakikisha huduma ya maji safi na kujisafi (WASH) kwa wanafunzi wote kwenye shule za wilaya za Adjumani na Arua nchini Uganda. Kisha anabisha hodi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC huko serikali imepatia wakimbizi na wenyeji ardhi ya ekari 500 kuimarisha kujitegemea, mkimbizi katoa shukrani. Jarida linasalia huko huko DRC kumulika juhudi za UNICEF kuona watoto wanasoma licha ya kuishi kwenye vituo vya ukimbizini. Makala inabisha hodi Tanzania, miundombinu ya kujikinga na magonjwa shuleni imeimarishwa kufuatia COVID-19 na mashinani tunarejea Adjumani huko Arua nchini Uganda, karibu!

Audio Credit
GRACE KANEIYA
Audio Duration
12'51"