Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 Aprili 2022

20 Aprili 2022

Pakua

Hii leo jaridani na Grace Kaneiya ni mada kwa kina ikimulika harakati za taasisi ya TAI nchini Tanzania ya kutumia michezo ya kuigiza, vikaragosi, au katuni za kwenye majarida au zenye sauti kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo haki, elimu na afya. Anold Kayanda amezungumza na Ian Tarimo, kiongozi wa taasisi hiyo ambaye alikuwa jijini New York, Marekani. Halikadhalika kuna habari kwa ufupi zikianzia masuala ya amani na usalama huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kisha Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR na kutatatishiwa huko Ukraine ambako Umoja wa Mataifa unapeleka jenereta za umeme kuhakikisha huduma za hospitali kwa wagonjwa hazikomi kutokana na mashambulizi yanayoaendelea. Mashinani tunabisha hodi nchini Somalia kwa mnufaika wa mradi wa maji uliofanikishwa na UNICEF. Karibu!

Audio Credit
GRACE KANEIYA
Audio Duration
13'28"