Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

28 JANUARI 2020

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

- Takriban watoto milioni 5 Sahel ya Kati watahitaji msaada wa kibinadamu wa haraka mwaka huu wa 2020 limesema shirika la kuhudumia watoto la UNICEF

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema machafuko yanayoendelea Darfur Magharibi nchini Sudan yamewalazimisha watu 11,000 kufungasha virano na kuingia nchi jirani ya Chad

-Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS na serikali ya Sudan Kusini wameanzisha kampeni ya kukabiliana na wizo wa mifugo

Sauti
10'56"

27 Januari 2020

Jaridani leo Januari 27, 2020 na Flora Nducha:

-Wakati dunia ikiadhimishamauaji ya maangamizi makuu au Holocaust Katibu Mkuu amesema, "Tunapowakumbuka waathirika wa Holocaust tuhakikishe uhalifu huo haturejei."

-Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema Lazima kuwe na uwajibikaji wa vifo vya mashambulizi ya anga Libya-UN

-Miji yenye mfumo bora wa elimu, ni mfano wa kuigwa-UNESCO 

Na katika makala ni kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye tiba ya asili

Na mashinani tunaelekea nchini Madagascar.

 

Sauti
14'14"

24 Januari 2020

Ni Ijumaa  ya Januari 24 mwaka 2020 kama kawaida leo ni mada kwa kina ambapo leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya elimu, tutaangazia harakati za uboreshaji wa elimu duniani kote na zaidi tutajikita nchini Tanzania kutathimini hatua zilizofikiwa tangu kutangazwa kwa elimu bila malipo. 

Sauti
10'25"

23 Januari 2020

 ICJ yaitaka Myanmar kuwalinda Warohingya dhidi ya mauaji ya kimbari. Vikosi vya upinzani Sudan Kusini vyaanza kujumuishwa kwenye jeshi la kitaifa. Dola bilioni 1 zahitajika kusaidia watu milioni 3 mwaka 2020 Somalia.

Sauti
11'26"

22 Januari 2020

Hii leo tunaanza na kauli ya Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa kuhusu changamoto 4 na suluhu 4 kwa ajili ya kuhakikisha mafanikio ya karne ya 21 hayafutiliwi mbali kisha tunakwenda Kigoma kumulika jinsi miradi ya Umoja wa Mataifa kwenye kilimo inavyoendelea kufuta kilimo cha "tangulia nakuja" hususan wilayani Kibondo, tumezungumza na Martine Kapaya.

Sauti
13'34"

21 JANUARI 2020

Shirika la Umoja wa Mataifa la kutokomeza Ukimwi, UNAIDS limesema afya bora si haki ya matajiri pekee, bali kila mtu. Jukwaa la kidijitali kukusanya takwimu kuhusu njaa na mzozo duniani lazinduliwa. Mkuu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Mark Lowcock amesema Umoja wa Mataifa utafanya kila uwezalo kuwasaidia wakimbizi Za’atari. 

Sauti
9'54"

20 JANUARI 2020

Kigori 1 kati ya 3 kutoka familia maskini hawajawai kwenda shule limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF. Mangariba watupa visu vya ukeketaji huko Sierra Leone.  Uvutaji tumbaku unaongeza hatari ya madhila baada ya upasuaji limeonya shirika la afya duniani WHO. 

Sauti
10'53"

16 JANUARI 2020

Katika Jarifada la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Watu milioni 45 katika nchi 16 za Kusini mwa Afrika maisha yao yako hatarini kutokana na njaa, na hatua za haraka za msaada zinahitajika limesema shirika la Umoja wa Matafa la mpango wa chakula duniani WFP

-Kimbunga Idai kilifungua macho ya madhila yanayowasibu watu wenye ulemavu nchini Zimbawe kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na elimu, UNESCO

Sauti
11'44"

14 JANUARI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Grace Kaneiya anakuletea 

-Dola milioni 477 zahitajika ili kunusuru maisha ya takriban watu laki tisa nchini Sudan kwa mahitaji ya kibinadamu kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR lililozindua ombi hilo leo mjini Khartoum 

-Ofisi ya miradi ya Umoja wa Mataifa, UNOPS kwa kushirikiana na Benki ya dunia pamoja na wadau wenyeji, wanafanya juhudi za kuboresha huduma mijini pamoja na nishati ya umeme kwa mamilioni ya watu wa Yemen.

Sauti
10'41"