Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

07 FEBRUARI 2020

Jaridani Februari 07, 2020 na Anold Kayanda. Ikiwa leo ni Ijumaa utasikia Habari kwa ufupi, mada kwa kina imejikita katika suala la ukeketaji tukiangazia nchini Tanzania ambako manusura mmoja anapambana kuhakikisha hakuna mtoto mwingine wa kike atakayekumbana na madhila haya. Na ikiwa leo ni Ijumaa tutasikia uchambuzi wa methali la wiki kutoka BAKIZA.

Sauti
10'23"

06 Februari 2020

Ukeketaji unaathiri wasichana na wanawake na gharama ya matibabu ni dola bilioni 1.4 kwa mwaka kimataifa imesema WHO, Mwaka mmoja baada ya makubaliano ya amani, mamilioni ya watoto CAR bado wako hatarini. Tangu nimeacha ungariba nimeshawaokoa wato takribani 150-Aliyeacha ungariba.

Sauti
10'15"

05 FEBRUARI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Anold Kayanda anakuletea
-UNHCR yaongeza hatua za kukabiliana na hali ya wakimbizi Sahel ghasia zikishika kasi
-Somalia inahitaji msaada wa kibinadamu wakati watu milioni 4.1 wakikabiliwa na kutokuwa na uhakika wa chakula
-UNESCO yasema asilimia 32 ya watu wa zaidi ya miaka 15 Nepali hawajui kusoma wala kuandika
-Makala yetu leo inatupeleka mkoani Kagera kumulika mchango wa wauguzi na wakunga
Na Mashinani tuko Afghanistan ambako UNICEF inapambana na utapiamlo

Sauti
11'41"

04 FEBRUARI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo kutoka Umoja wa Mataifa arnold Kayanda anakuletea
-Shirika la afya ulimwenguni WHO limetaja hatua za kunusu maisha ya watu milioni 7 kutokana na saratani
-Watu zaidi ya 520,000 wamefurushwa makwao Syria katika miezi miwli iliyopita kutokana na machafuko Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo
-Baa la njaa lainyemelea Sudan Kusini WFP yaonya bila msaada na fedha mamilioni ya watu watakuwa hatarini
-Makala yetu leo inatupeleka zanzibar kumulika mchango wa wauguzi na wakunga
Na Mashinani tuko Yemen ambako nishati ya jua au Sola imeleta nuru

Sauti
12'3"

31 JANUARI 2020

Jaridani Januari 31, 2020 na Arnold Kayanda. Ikiwa leo ni Ijumaa utasikia Habari kwa ufupi, mada kwa kina imejikita katika mlipuko wa virusi vya corona tukiangazia nchini Kenya ambako kuna mgonjwa anayefanyiwa uchunguzi kuthibitisha iwapo ana virusi vya corona baada ya kuwasili kutoka China na dalili za homa. Na ikiwa leo ni Ijumaa tutasikia uchambuzi wa neno la wiki kutoka BAKITA.

Sauti
11'4"

30 JANUARI 2020

Jaridani Januari 30, 2020 na Flora Nducha, pata habari ikiwemo Shirika la mpango wa chakula duniani limesema uwepo wa ufadhili wa kuaminika utarahisisha uwasilishaji wa misaada. Mwakilishi wa UN wa vijana atembelea vijana kwenye kambi ya kuhifadhi wakimbizi wa ndani nchini Sudan Kusini, na nchini Niger, ujenzi wa nyumba kwa ajili ya wakimbizi na wenyeji na UNHCR na wadau ni habari njema. Makala tunaangazia mlipuko wa nzige, mashinani tupo nchini Tanzania.

Sauti
12'

28 JANUARI 2020

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

- Takriban watoto milioni 5 Sahel ya Kati watahitaji msaada wa kibinadamu wa haraka mwaka huu wa 2020 limesema shirika la kuhudumia watoto la UNICEF

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema machafuko yanayoendelea Darfur Magharibi nchini Sudan yamewalazimisha watu 11,000 kufungasha virano na kuingia nchi jirani ya Chad

-Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS na serikali ya Sudan Kusini wameanzisha kampeni ya kukabiliana na wizo wa mifugo

Sauti
10'56"

27 Januari 2020

Jaridani leo Januari 27, 2020 na Flora Nducha:

-Wakati dunia ikiadhimishamauaji ya maangamizi makuu au Holocaust Katibu Mkuu amesema, "Tunapowakumbuka waathirika wa Holocaust tuhakikishe uhalifu huo haturejei."

-Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema Lazima kuwe na uwajibikaji wa vifo vya mashambulizi ya anga Libya-UN

-Miji yenye mfumo bora wa elimu, ni mfano wa kuigwa-UNESCO 

Na katika makala ni kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye tiba ya asili

Na mashinani tunaelekea nchini Madagascar.

 

Sauti
14'14"

24 Januari 2020

Ni Ijumaa  ya Januari 24 mwaka 2020 kama kawaida leo ni mada kwa kina ambapo leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya elimu, tutaangazia harakati za uboreshaji wa elimu duniani kote na zaidi tutajikita nchini Tanzania kutathimini hatua zilizofikiwa tangu kutangazwa kwa elimu bila malipo. 

Sauti
10'25"