Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 Januari 2020

22 Januari 2020

Pakua

Hii leo tunaanza na kauli ya Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa kuhusu changamoto 4 na suluhu 4 kwa ajili ya kuhakikisha mafanikio ya karne ya 21 hayafutiliwi mbali kisha tunakwenda Kigoma kumulika jinsi miradi ya Umoja wa Mataifa kwenye kilimo inavyoendelea kufuta kilimo cha "tangulia nakuja" hususan wilayani Kibondo, tumezungumza na Martine Kapaya. Huko Yemen nako UNICEF yachukua hatua kukabilia homa ya vichomi miongoni mwa watoto na  makala tunakwenda Uganda ambako kijana mmoja amechukua hatua ya kijasiri kunufaika na mradi wa uchimbaji mafuta nchini humo na mashinani ni nchini Pakistani ambako FAO imeleta nuru kwa wakulima kupitia mafunzo mahsusi. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
13'34"