Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 JANUARI 2020

14 JANUARI 2020

Pakua

Katika Jarida la Habari hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Grace Kaneiya anakuletea 

-Dola milioni 477 zahitajika ili kunusuru maisha ya takriban watu laki tisa nchini Sudan kwa mahitaji ya kibinadamu kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR lililozindua ombi hilo leo mjini Khartoum 

-Ofisi ya miradi ya Umoja wa Mataifa, UNOPS kwa kushirikiana na Benki ya dunia pamoja na wadau wenyeji, wanafanya juhudi za kuboresha huduma mijini pamoja na nishati ya umeme kwa mamilioni ya watu wa Yemen.

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP linawasaidia wanawake wavuvi nchini Ecuador kukidhi mahitaji ya chakula kutokana na kuathirika vibaya na mabadiliko ya tabianchi.

-Makala yetu leo inabisha hodi Sake Kivu ya Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwa mwanamke muathirika wa ukatili wa kijinsia na kingono ambaye sasa ni mjasiriamali kwa msaada wa mradi wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCO.

-Na mashinani utamsikia mtoto wa miaka 11 kutoka Zambia alienufaika na program ya elimu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Audio Credit
UN News/Grace Kaneiya
Sauti
10'41"