Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Watu waliotawanywa na machafuko wakitembea kurejea eneo la Savo mapema asubuhi karibu baada ya kupata hifadhi katika mji wa karibu wa Bule nchini DRC
© UNHCR/Hélène Caux

Hatua za haraka zahitajika huku idadi ya wanaolazimika kuhama makwao ikifikia milioni 110: UNHCR

Vita nchini Ukraine, pamoja na migogoro mingine na machafuko yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi, vinamaanisha watu wengi zaidi kuliko wakati mwingine wowote walifurushwa makwao mwaka jana, na hivyo kuongeza udharura wa kuchukua hatua za haraka za Pamoja kupunguza janga hilo la kimataifa limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. 

UN Women/BrunoDemeocq

Bahari ni sehemu ya suluhisho la matatizo lukuki katika jamii - FAO

Wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya habari duniani hapo kesho Juni nane shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limesema ni vyema jamii kuzingatia afya ya baharí kwani umuhimu wake kamwe hauwezi kupuuzwa.

Bahari, ni makazi ya asilimia 80 ya majani ya wanyama, ambayo yanatumika kama chanzo muhimu cha wananchi kujipatia riziki na pia lishe kwa mamilioni ya watu ulimwenguni.

Sauti
2'47"

06 JUNI 2023

Jaridani hii leo tunaangazia ni mada kwa kina na nakupeleka mwambao wa Ziwa Tanganyika nchini Tanzania, hususan mkoani Rukwa ambako huko utasikia harakati za Umoja wa Mataifa za kujumuisha wanawake kwenye uvuvi. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Nishati jadidifu, mabadiliko ya tabianchi na afya. Katika mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini kusikia ni kwa jinsi gani vijana wanachangia katika mchakato wa utengenezaji wa katiba ukielekea uchaguzi mkuu nchini humo.

Sauti
13'27"