Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

UN News

Tunaelimisha wanafunzi na vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi - Madina Jubilate Kimaro

Wiki hii hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa tathmini ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs kuona wapi nchi wanachama, kampuni, watu binafsi wamefikia kusongesha maendeleo hayo yanayofikia ukomo mwka 2030. Vijana nao walikuwa na siku zao mbili za kuelezea wanafanya nini kule waliko na wanataka nini kifanyike kusongesha malengo hayo likiwemo namba 13 la tabianchi. Miongoni mwa vijana walioshiriki ni Madina Jubilate Kimaro, Balozi wa Mazingira wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF nchini Tanzania.

Sauti
6'24"
Viongozi wa mataifa, wafanyabiashara na mashirika ya kiraia walikusanyika mjini New York kwa ajili ya Mkutano wa Kilele wa Matarajio ya Hali ya Hewa ulioandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
© UN News/Anton Uspensky

Muungano wa mabadiliko ya tabianchi wadai hatua, huku Guterres akionya Ubinadamu umefungua milango ya kuzimu

"Joto la kupindukia linaleta madhara ya kutisha duniani ", kwa mujibu wa mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa akizungumza leo katika mkutano wa kwanza kabisa wa ngazi ya juu wa matarajio kuhusu mabadiliko ya tabianchi mbele ya mbele ya muungano wa kimataifa wa kuchagiza hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ulijumuisha wachagizaji, watendaji, wanasiasa, wafanyabiashara, mashirika ya kimataifa na viongozi wa asasi za kiraia waliokusanyika New York kandoni mwa mjadala wa Baraza kuu UNGA78.

UN News/Flora Nducha

Tunakumbatia wito wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo - Vijana Bongoyo Tanzania

Wakati macho na masikio ya Dunia yakielekezwa hapa New York Marekani kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakaoanza Jumatatu wiki ijayo kujadili mada mbalimbali ikiwemo hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi , tunaelekea Tanzania ambako katika pitapita zake, Flora Nducha alipokuwa jijini Dar es Salaama alikutana na mmoja wa vijana wajasiriamali kwenye kisiwa cha Bongoyo waliokumbatia wito wa kupambana na jinamizi la mabadiliko ya tabianchi, akamweleza  Flora kuwa mbali ya kujipatia kipato kutokana na utalii endelevu ana jukumu kubwa pamoja na baadhi ya vijana wenzie la kul

Sauti
4'26"
Mafuriko yamekumba maeneo ya kaskazini mashariki mwa Libya.
© National Meteorological Centre, Libya

Takriban watu 3, 000 wamekufa na 10,000 hawajulikani waliko kufuatia mafuriko Libya:WMO/WHO/IOM/IFRC

Mafuriko makubwa yaliyoikumba Libya tarehe 10 September yamesababisha maafa ikiwemo vifo vya takriban watu 3,000 na wengine zaidi ya 10,000 kutojulikana waliko Mashariki mwa nchi hiyo  kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu IFRC na mwezi mwekundu.