Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

06 JUNI 2023

06 JUNI 2023

Pakua

Jaridani hii leo tunaangazia ni mada kwa kina na nakupeleka mwambao wa Ziwa Tanganyika nchini Tanzania, hususan mkoani Rukwa ambako huko utasikia harakati za Umoja wa Mataifa za kujumuisha wanawake kwenye uvuvi. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Nishati jadidifu, mabadiliko ya tabianchi na afya. Katika mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini kusikia ni kwa jinsi gani vijana wanachangia katika mchakato wa utengenezaji wa katiba ukielekea uchaguzi mkuu nchini humo.

  1. Ripoti mpya iliyozinduliwa leo kuhusu hatua zilizopigwa katika ufikiaji wa lengo namba 7 la maendeleo endelevu SDGs ifikapo mwaka 20230 lihusulo nishati, inasema pengo la nishati duniani bado linaendelea kwani watu milioni 675 hawana umeme, huku watu wengine bilioni 2.3 wanategemea nishati za kupikia ambazo ni hatari kwa afya zao na mazingira.    
  2. Umoja wa Mataifa umezindua mradi wa miaka miatatu  wa kuimarisha mnepo wa jamii dhidi ya mabadiliko ya tabianchi mkoani Kigoma nchini Tanzania ambako mamia kwa maelfu ya wakimbizi wanahifadhiwa.
  3. Na kuelekea siku ya usalama wa chakula duniani hapo kesho Juni 7 mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO na la mpango wa chakula duniani WFP kwa kushirikiana na sekretarieti ya Codex Alimentarius wamesema kila siku takriban watu milioni 1.6 duniani kote wanaugua kutokana na kula chakula kisicho salama.
  4. Na katika mashinani Elizabeth Acu, Mwanaharakati wa vijana ambaye pia ni mwanauchumi nchini Sudan Kusini, anaeleza jukumu la vijana katika uundaji na uimarishaji wa katiba, na pia changamoto zinazoikumba nchi hiyo huku mchakato wa uchaguzi mkuu unapokaribia.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
13'27"