Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupunguza taka za plastiki kunahitaji mabadiliko makubwa: UNEP Ripoti

Uchafu wa baharini, ikiwa ni pamoja na plastiki, karatasi, mbao, chuma na nyenzo nyingine za viwandani hupatikana kwenye eneo la pwani duniani kote na katika vilindi vyote vya bahari.
Unsplash/Naja Bertolt Jensen
Uchafu wa baharini, ikiwa ni pamoja na plastiki, karatasi, mbao, chuma na nyenzo nyingine za viwandani hupatikana kwenye eneo la pwani duniani kote na katika vilindi vyote vya bahari.

Kupunguza taka za plastiki kunahitaji mabadiliko makubwa: UNEP Ripoti

Tabianchi na mazingira

Uchafuzi wa taka za plastiki unaweza kupunguzwa kwa asilimia 80 ifikapo mwaka 2040 ikiwa nchi na makampuni yatafanya mabadiliko ya kina ya sera na masoko kwa kutumia teknolojia zilizopo, kulingana na ripoti mpya  iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP.

Ripoti hiyo imetolewa kabla ya duru ya pili ya mazungumzo yatakayofanyika mjini Paris kuhusu makubaliano ya kimataifa ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira utokanao na plastiki duniani na inaeleza ukubwa na asili ya mabadiliko yanayohitajika ili kukomesha uchafuzi wa plastiki na kuunda uchumi endelevu.

Ripoti hiyo” Kiini: Kukomesha uchafuzi wa Plastiki na kuunda uchumi endelevu duniani” inatoa uchanganuzi unaozingatia suluhu za kushughulikia mazoea halisi ya ulimwengu, mabadiliko ya masoko na sera zinazoweza kuongoza fikra na sera za serikali za kuchua hatua za ushirikiano.

Inger Andersen, mkurugenzi mtendaji wa UNEP amesema "Njia tunazozalisha, kutumia na kutupa plastiki huchafua mifumo ya ikolojia, na kuleta hatari kwa afya ya binadamu na pia kuharibu hali ya hewa. Ripoti hii ya UNEP inatoa ramani ya njia ya kupunguza hatari hizi kwa kutumia mbinu ya mzunguko au kurejeleza ambayo inazuia plastiki kutoka kwenye mifumo ya ikolojia na miili yetu na kuziweka katika uchumi. Kwa kufuata ramani hii, ikiwa ni pamoja na wakati wa mazungumzo juu ya makubaliano ya kupambana na uchafuzi wa plastiki, tunaweza kupata ushindi muhimu wa kiuchumi, kijamii na kimazingira”.

Nchini Kenya, vifaa vya ujenzi vya bei nafuu, kama vile matofali vinatengenezwa na taka za plastiki na mchanga.
UNEP
Nchini Kenya, vifaa vya ujenzi vya bei nafuu, kama vile matofali vinatengenezwa na taka za plastiki na mchanga.

Mapendekezo ya ripoti

Ili kupunguza uchafuzi wa plastiki kwa asilimia 80 duniani kote ifikapo 2040, ripoti inapendekeza kama hatua ya kwanza ya kuondoa plastiki zenye matatizo na zisizo za lazima ili kupunguza ukubwa wa tatizo.

Baadaye, ripoti hiyo inataka mabadiliko matatu kwenye soko, yakilenga utumiaji tena, urejelezaji, na upangaji upya wa bidhaa na matumizi mbalimbali:

Utumiaji tena: Kukuza chaguo za utumiaji ten awa bidhaa kama vile chupa zinazoweza kutumika tena, vifungashio vya chakula, au mifumo ya kuweka au kuchukua tena, kunaweza kusababisha kupungua kwa 30 ya uchafuzi wa plastiki nyumbani hadi  kufikia mwaka 2040.

Ili kutambua uwezo huu, serikali lazima zisaidie kufanya bidhaa zinazoweza kutumika tena kuwa za kiuchumi zaidi.

Urejelezaji: Kwa kuhakikisha kuwa kuchakata tena kunakuwa shughuli dhabiti na yenye faida, inawezekana kupunguza uchafuzi wa plastiki kwa asilimia 20 ya ziada ifikapo 2040.

Kuondoa ruzuku za mafuta ya visukuku, kutumia miongozo ya usanifu inayohimiza urejeleaji, na hatua zingine zinaweza kuongeza sehemu ya kiuchumi na plastiki inayoweza kutumika tena kutoka asilimia 21 hadi asilimia 50.

Uelekezaji kwingine na matumizi mbalimbali: Kubadilisha kwa uangalifu bidhaa kama vile vifuniko vya plastiki, mifuko na vifungashio na bidhaa zilizotengenezwa kutokana na nyenzo nyingine kama vile karatasi au nyenzo zinazoweza kutengenezwa kunaweza kupunguza uchafuzi wa plastiki kwa  asilimia 17 ya ziada.

Ripoti imesisitiza kuwa hata kama hatua zilizotajwa hapo juu zitatekelezwa, bado itakuwa muhimu kudhibiti kwa usalama tani milioni 100 za plastiki kutoka kwa matumizi ya mara moja, bidhaa za muda mfupi kila mwaka ifikapo mwaka 2040, pamoja na uchafuzi wa plastiki uliokusanywa kwa miaka kufikia idadi kubwa. Kwa hili, inawezekana kuunda na kuanzisha viwango vya kubuni na vya usalama kuhusiana na utupaji wa taka za plastiki zisizoweza kutumika tena, na kuwafanya wazalishaji kuwajibika kwa bidhaa zinazotoa chembechembe za plastiki, miongoni mwa wengine.

Matofali ya plastiki yanatengenezwa kwa takamali za plastiki katika kiwanda cha Abidjan, Côte d'Ivoire.
© UNICEF/Milequem Diarassouba
Matofali ya plastiki yanatengenezwa kwa takamali za plastiki katika kiwanda cha Abidjan, Côte d'Ivoire.

Matrilioni ya dola kuokolewa

Katika kiwango cha kimataifa, hatua ya kuelekea uchumi endelevu ingeokoa akiba ya dola bilioni 1.270, kwa kuzingatia gharama na mapato yanayohusiana na kuchakata tena taka za plastiki.

Zaidi ya hayo, dola trilioni 3.25 za ziada zingeokolewa kupitia gharama za nje zitakazoepukwa katika afya, hali ya hewa, uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa mfumo wa ikolojia wa baharini, na gharama za kesi.

Mpito huu pia ungesaidia kuundwa kwa nafasi za kazi 700,000 ifikapo mwaka 2040, hasa katika nchi za kipato cha chini, na kuboresha kwa kiasi kikubwa maisha ya mamilioni ya wafanyakazi katika sekta isiyo rasmi.

Gharama za uwekezaji zinazohusiana na mabadiliko ya utaratibu yaliyopendekezwa ni ya juu, lakini bado ni chini ya matumizi ambayo yatahitajika ikiwa mabadiliko haya ya utaratibu hayatatokea, kwani n idola bilioni 65 bilioni dhidi ya dola bilioni 113.

Uwekezaji katika teknolojia

Ripoti inasema sehemu kubwa ya jumla hii  ya fedha inaweza kuchangishwa kwa kuelekeza uwekezaji uliopangwa kwenda kwenye vifaa vipya vya uzalishaji ambayo haitakuwa muhimu tena ikizingatiwa kupunguzwa kwa hitaji la plastiki au kwa kuweka ushuru wa utengenezaji wa plastiki mpya  kwa faida ya miundombinu muhimu.

“Lakini inasema ripoti wakati unatutupa mkono  na kucheleweshwa kwa miaka mitano kunaweza kusababisha kutolewa kwa tani zingine milioni 80 za uchafuzi wa plastiki ifikapo 2040.”

Gharama kubwa zaidi za uchumi unaoweza kutumika na uchumi endelevu unahusiana na uendeshaji.

Iwapo kanuni zitahakikisha kuwa plastiki zimetengenezwa kwa kuzingatia uendelevu mipango iliyopanuliwa ya uwajibikaji wa mzalishaji inaweza kulipia gharama za uendeshaji za kuhakikisha mzunguko wa mfumo, kwa kuwataka wazalishaji kufadhili ukusanyaji, urejelezaji na utupaji wa uwajibikaji wa mwisho wa maisha wa bidhaa za plastiki.

Wakazi wa eneo la ufukwe wa watamu wakifanya  usafi wa ufukwe pamoja  mashirika ya ulinzi wa mazingira
Picha UNEP/Cyril Villemain
Wakazi wa eneo la ufukwe wa watamu wakifanya usafi wa ufukwe pamoja mashirika ya ulinzi wa mazingira

Kuweka vigezo vya kawaida

Sera zilizokubaliwa kimataifa zinaweza kusaidia kushinda changamoto za upangaji wa kitaifa na hatua za ushirikiano, kukuza uchumi endelevu wa kimataifa na unaostawi wa plastiki, kufungua fursa za biashara na kuunda nafasi za ajira.

Huenda zikahusisha vigezo vya kawaida vya bidhaa za plastiki zinazoweza kupigwa marufuku, msingi wa maarifa wa kimataifa, sheria za viwango vya chini vya utendakazi wa mipango ya wajibu wa mtayarishaji ulioongezwa na viwango vingine.

Ripoti ya UNEP inapendekeza kuzingatia ujumuishaji wa mfumo wa fedha wa kimataifa katika sera za kimataifa ili kuruhusu nyenzo zilizorejelewa kushindana kwenye uwanja sawa na nyenzo mbichi, kuunda uchumi wa viwango katika suluhu zilizopendekezwa, na kuweka mifumo ya ufuatiliaji na mifumo ya ufadhili.

Ripoti imesisitiza kwamba “Ni muhimu watunga sera wachukue mbinu ambayo inashughulikia vyombo vya udhibiti na sera zinazolenga vitendo vinavyohusiana na mzunguko wa maisha wa plastiki, kwani wanaimarishana ili kufikia lengo la kubadilisha uchumi. Kwa mfano, sheria za usanifu zinazolenga kufanya bidhaa ziweze kutumika tena kiuchumi zinaweza kuunganishwa na malengo ya maudhui yaliyorejelewa ya bidhaa na faida za kodi zinazolenga mitambo ya kuchakata tena plastiki hizo.”

Ripoti hiyo pia inajadili sera mahususi, ikiwa ni pamoja na muundo, usalama na viwango vya plastiki vinayoweza kuoza, malengo ya chini ya urejeleaji, mifumo iliyopanuliwa ya uwajibikaji wa wazalishaji, kodi, marufuku, mikakati ya mawasiliano, ununuzi wa umma na uwekaji nembo.