Idhaa ya Kiswahili ya UN yashinda tuzo ya kimataifa ya Kiswahili ya Shaaban Robert
Nchini Tanzania hii leo Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, UN NEWS KISWAHILI imeibuka mshindi wa tuzo ya kimataifa ya kiswahili ya Shaaban Robert katika kategoria ya ukuzaji wa misamiati. Hii ni mara ya kwanza kwa kipengele hicho kutolewa na kwenye tuzo hizo ambapo tumemuuliza Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, mmoja wa waaandaji wa tuzo hizo utaratibu wa ushindanishi.