Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Wahudumu wa afya baada ya kupokea chanjo dhidi ya COVID-19 katika hospitali nchini India.

Mashirika ya UN yaunga kampeni ya chanjo dhidi ya COVID-19 India  

UNICEF/Vinay Panjwani
Wahudumu wa afya baada ya kupokea chanjo dhidi ya COVID-19 katika hospitali nchini India.

Mashirika ya UN yaunga kampeni ya chanjo dhidi ya COVID-19 India  

Afya

India imeanza kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni kubwa zaidi duniani ya utoaji chanjo dhidi ya virusi vya corona au COVID-19, ikipeleka maelfu kwa maelfu ya wahudumu wa afya wenye ujuzi na kwa msaada wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.

Tarehe 16 Januari siku ya kwanza ya kamepni hiyo chanjo 207,229 zilitolewa katika sehemu mbalimbali za India nchi ambayo ni miongoni mwa zilizoathirika vibaya kabisa na janga hilo la COVID-19 ambapo watu zaidi ya milioni 10 wameambukizwa na 150,000 wameshapoteza maisha hadi sasa.  

Madakatari na wahudumu wa afya ni wa kwanza kupokea chanjo dhidi ya COVID 19 nchini India
© UNICEF/Vinay Panjwani
Madakatari na wahudumu wa afya ni wa kwanza kupokea chanjo dhidi ya COVID 19 nchini India

Tumetoa msaada wa kiufundi kwa serikali ya India kwa ajili ya kuandaa muongozo na vifaa vya mafunzo kwa ajili ya program za majimbo na wilaya kwa mameneja na watoaji chanjo, na pia kuanzisha mifumo ya kufuatilia na uwajibikaji,” amesema Roderico H. Ofrin, mwakilishi wa WHO nchini India. 

Ameongeza kuwa Maafisa wa WHO huko mashinani wamewezesha uangalizi wa hali ya juu wa chanjo hiyo kupitia mikutano ya kikosi kazi maalum katika ngazi ya jimbo na ya wilaya ambayo inaongozwa na makatibu wakuu wa afya katika ngazi ya jimbo na mhakimu katika ngazi ya wilaya.” 

Kwa mujibu wa duru za Habari takriban wahudumu wa afya milioni 10 wanalengwa kuchanjwa katika duru ya kwanza ya kampeni hiyo , wakifuatiwa na wahudumu wengine wa msitari wa mbele kama vile polisi, vikosi vya ulinzi na wafanyakazi wa manispaa, huku lengo likiwa kuwachanja watu milioni 300 ifikapo mwezi agosti mwaka huu. 

Kusaidia maandalizi 

Kabla ya kuanza kwa kampeni hii mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yalisaidia kwa kina maandalizi. Kwa upande wake WHO ilishiriki katika mchakato wa majaribio ya kuigiza na kuwapa muongozo na ushauri wa kutoa chanjo hiyo, uandikishaji wa watakaopokea chanjo pamoja na kutoa taarifa kwa watakaopokea chanjo hiyo na yale yatakayojitokeza kufuatia chanjo hiyo. 

WHO pia imeshirikiana kwa karibu na serika;li na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP katika kutoa taarifa za papo kwa papo na kutatua matatizo wakati yanapojitokeza katika maeneo ambako chanjo inatolewa amesema Dkt. Ofrin. 

Katika ngazi ya majimbo WHO imesaidia utekelezajio na ufuatiliaji wa sera za afya, kama vile kuanzisha viwango vya kawaida vya operesheni , kuandaa taarifa za kiufundi na kutoa mifano bora kutoka katika maeneo mengine nchini India na pia katika mataifa mengine. 

Familia zikipokea chanjo na ushauri katika kijiji walichozingatia umbali unaohitajika cha afya na lishe Gujarat, India.
UNICEF/Panjwani
Familia zikipokea chanjo na ushauri katika kijiji walichozingatia umbali unaohitajika cha afya na lishe Gujarat, India.

 

Taarifa za kuaminika 

Kama WHO pia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limesaidia katika upande wa mawasiliano na juhudi za uelimishaji ili kuhakikisha usambazaji wa taarifa sahihi kwa wadau na jamii. 

Shirika hilo pia limesaidia kuwapa mafunzo wahudumu wa afya ya kuzuia na kudhibiti maambukizi na kutoa msaada wa kisaikolojia kwa watoto na watu wanaowahudumia. 

Mbali ya kusaidia moja kwa moja mchakato wa utoaji chanjo hiyo , mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na progamyu zake za kusaidia jamii zilizo hatarini zaidi ambazo zimeathirika na COVID-19 na athari zinazowakabili za kiuchumi na kijamii. 

Kwa mfano shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP limekuwa likiyasaidia mashirika yasiyo ya kiserikali au NGOs kubaini na kusajili kaya zisizojiweza 19,000 na kugawa vifurushi vya chakula , huku shirika la idadi ya watu duniani UNFPA limeendesha programu za uelimishaji hasa katika masuala ya afya ya uzazi na kuzuia ukatili wa kijinsia kwa niaba ya watu milioni 30 walio hatarini. 

Mfanyakazi nchini India ambaye anataka kupata chanjo dhidi ya COVID-19.
UNICEF India/ Ruhani Kaur
Mfanyakazi nchini India ambaye anataka kupata chanjo dhidi ya COVID-19.

Mambo matatu ya kuzingatia 

Ingawa mchakato wa chanjo unaendeklea kuhakikisha watu wanakuwa makini na kujikinga dhidi ya COVID-19 ni suala linalosalia kuwa muhimu sana kuliko wakati mwingine wowote. 

Dkt. Ofrin wa WHO amewataka wahudumu wa afya kuwa makini zaidi katika kufuatilia wagonjwa, kuchunguza, kuwatenga, kuwahudumia na kuwaweka karantini washukiwa ili kuvunja mzunguko wa maambukizi . 

Daktari huyo pia amehimiza kuhusu masuala matatu muhimu ya kuzingatia ambayo ni “Vaa barako, Nawa mikoni yako na Hakisha umbali kati ya mtu na mtu. Hatua hizi lazima ziendelee ili kukomesha kusambaa kwa COVID-19. Sisi kama watu binafsi na jamii ni lazima tushirikiane na serikali kuokoa maisha na uchumi kwa kulinda afya na maisha yetu.” Ameongeza.