Mukhisa Kituyi atangaza kujiuzulu Februari 15, Katibu Mkuu amshukuru kwa mchango wake

19 Januari 2021

Katibu Mkuu wa kamati ya Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi amemwelezea Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres  kuhusu nia yake ya kujiuzulu kutoka nafasi hiyo kuanzia tarehe 15 mwezi ujao wa Februari.

Katibu Mkuu Guterres amemshukuru bwana Kituyi kwa kazi yake na dhamira ykae kwa majukumu aliyopewa kama mfanyakazi wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa. 

Katika kipindi alichohudumu kwenye UNCTAD alichagiza kazi juu ya biashara, uwekezaji, fedha na teknolojia na kutoa suluhu kwa ajili ya changamoto nyingi zinazozikabili nchi zinazoendelea hususan nchi maskini na zile zilizo hatarini. 

Naibu Katibu Mkuu wa UNCTA, Bi. Isabelle Durant wa Ubelgiji atakaimu nfasai hiyo wakati Katibu Mkuu akianza mchakato wa kuajiri mtu mwingine kwa ushirikiano n anchi wanachama, kwa ajili ya kupata mtu wa kuchukua nafasi ya Dkt. Kituyi.  

Dkt. Kituyi kutoka Kenya ameshika nafasi hiyo kuanzia Septemba 2013. Nchini mwake ameshika nyadhifa mbali mbali serikalini ikwemo waziri wa biashara na viwanda kati ya mwaka 2002 hadi 2007. 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud