Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Raia wa kiarabu na kiisrael akionesha kadi yake ya kudhibitisha amepata chanjo ya COVID-19
Mohamed Yassin

Kuelekea kuhifadhi taarifa za chanjo ya Covid-19 kidijitali, WHO yatoa mwongozo

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema ingawa haliungi mkono mahitaji ya uthibitisho wa chanjo ya COVID-19 ili mtu kuweza kusafiri lakini katika mazingira mengine kulingana na tathmini ya hatari ya nchi zinazohusika, taarifa kuhusu chanjo dhidi ya COVID-19 zinaweza kutumika kupunguza mahitaji ya karantini au upimaji wakati wa kuwasili katika nchi hizo.

Sauti
1'43"
Kilimo nchini Bangladesh
© WFP/Sayed Asif Mahmud

Mradi wa umwagiliaji wa sola wawanufaisha wakulima na kuokoa mazingira Bangladesh:FAO 

Nchini Bangladesh uhaba wa maji unatishia uzalishaji wa kilimo na maisha ya wakulima hasa kutokana na kutokuwa na mifumo bora ya uwagiliaji ambayo inasababisha upotevu wa maji. Lakini sasa changamoto hizo zinageuka historia baada ya shirika la chakula na kilimo FAO kuanzisha mradi wa mifumo bora ya umwagiliaji inayotumia nishati ya jua au sola kunusuru wakulima na mazingira.

Sauti
2'37"
Dr.Alinda Mashiku

Penye nia pana njia kama nimefika NASA nawe utaweza: Mhandisi Dkt.Alinda Mashiku 

Mwanamke Mtanzania angara kituo cha safari za anga cha Marekani NASA  tawi la Goddard mjini Maryland lililojikita na ufuatiliaji wa safari za satellite. Dkt. Alinda Mashiku ambaye amekuwa NASA kwa miaka minane sasa anasema ilimchukua miaka 12 hadi kuajiriwa NASA kama mhandisi na sasa pia ni meneja wa kitengo cha kuhakikisha satellite zonazokwenda angani hazigongani. Je anahisi vipi kuwa miongoni mwa wanawake wachache wahandisi NASA na safari yake ilianza vipi? Kufahamu yote hayo na mengine mengi ungana na Flora Nducha wa UN News Kiswahili aliyeketi na kuzungumza naye katika makala hii  

Sauti
13'39"