Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuzo za kimataifa za  lugha ya Kiswahili za Shaaban Robert kutolewa kesho Tanzania

Tuzo za kimataifa za  lugha ya Kiswahili za Shaaban Robert kutolewa kesho Tanzania

Pakua

Nchini Tanzania kesho Jumatano kunatolewa tuzo na nishani za kimataifa za lugha ya Kiswahili za Shaaban Robert. Tukio hilo litafanyika kwenye mji mkuu wa taifa hilo la Afrika Mashariki, Dodoma, ambapo tukio linaleta pamoja washiriki na manguli na wabobezi wa lugha ya Kiswahili kutoka maeneo mbalimbali duniani, na litahusisha pia viongozi waandamizi wa serikali na mashirika ya kitaifa na kimataifa. Lakini tuzo hizo zilianzia wapi? Na ni nini mantiki yake? Ahimidiwe Olotu wa kituo cha Habari za Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam ambaye sasa yuko Dodoma, amepata fursa ya kuzungumza na Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa Tanzania, BAKITA, waandaaji wa tuzo hizo.
 

Audio Duration
6'
Photo Credit
UNIC/Ahimidiwe Olotu