Athari ya COVID-19 kwenye utalii zinaweza kusababisha pigo la dola trilioni 4 kwa uchumi wa dunia: Ripoti ya UN
Athari za janga la corona au COVID-19 katika sekta ya utalii linaweza kusababisha kupotea kwa zaidi ya dola trilioni 4 kwa uchumi wa dunia, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo kwa pamoja na shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD na shirika la Umoja wa Mataifa la utalii UNWTO.