Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR inasikitishwa na ukiukaji wa haki za binadamu Haiti

Siku tatu baada ya maandamano, watu wamekimbia mji mkuu.
MINUJUSTH/Leonora Baumann
Siku tatu baada ya maandamano, watu wamekimbia mji mkuu.

OHCHR inasikitishwa na ukiukaji wa haki za binadamu Haiti

Haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR, imeelezea wasiwasi wake kuhusu kuendelea kwa ukosefu wa usalama, umaskini, ukosefu wa usawa na kuongezeka kwa uhasama wa kisiasa ambao huenda ukachochea ghadhabu kutoka kwa umma ambayo itafuatiwa na kukandamizwa na polisi na ukiukaji wa haki za binadamu. 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi, msemaji wa OHCHR, Martha Hurtado amesema katika miezi michache iliyopita kumekuwa na utekaji nyara kwa aji ya kuitisha fidia, mashambulizi kutoka kwa makundi aliyojihami katika mitaa wanayohisi ni maadui na kuenea kwa ukosefu wa usalama katika mazingira ya kutowajibishwa. Kwa upande mwingine uhasama wa kisiasa umezuka kwa ajili ya mvutano kuhusu uchaguzi na kura ya maoni kuhusu katiba iliypendekezwa na serikali. 

Bi Hurtado ameongeza kwamba wito wamaandamano umeongezeka nai i inazua wasiwasi wa ukiukaji wa haki za binadamu na vikosi vya usalama wakati wa maandamano kama ilivyokuwa mwaka 2018 na 2019 na pia wakati wa maandamano ya Oktoba na Novemba mwaka jana. 

Ukiukaji wa haki za binadamu umeorodheshwa katika ripoti ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Matiafa nchini Haiti na ofisi ya haki za biandamu ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo. Ripoti inaonyesha ukiukaji wa hali za binadamu bila uwajibishaji na ukiukaji wa haki za watu waliokusanyika kwa amani . 

OHCHR imetoa wito kwa mamlaaka nchini Haiti kuchukua hatua kukabiliana na mizizi iliyochochea maandamano ikiwemo kutowajibishwa, madai ya ufisadi, umasikini, ukosefu wa usawa, huduma finy za kijamii na changamoto zinazokwamisha wahaiti kufurahi haki zao za kiuchumi na kijamii. 

OHCHR imekaribisa hatua ya polisi la kitaifa kubadili mienendo iliyoripotiwa kwenye ripoti ikiwemo kuhakikisha kwamba polisi wasimamizi wa maandamano wanapokua mafunzo. 

OHCHR imeelezea utayari wake kusaidia mamlaka kulinda haki za binadamu za kimataifa na kuendela kufanya kazi katika kufungua ofisi nchini humo.