Makamanda walichagua wanawake wa kuwaoa, wasiochaguliwa walibakwa na wapiganaji- Ripoti
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeorodhesha mateso kwa raia wa kawaida katika eneo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini ambapo watu 900 walitekwa na wengine 24,000 walilazimishwa kukimbia makazi yao kutokana na kuongezeka kwa ghasia kati ya mwezi Aprili na Agosti mwaka huu kabla ya makubaliano ya amani nchini humo.