Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlo wa dola 1.20 New York, wamgharimu mkazi wa Sudan Kusini dola 349- WFP

Mlo wa dola 1.20 New York, unagharimu mkazi wa Sudan Kusini dola 349.
UN News/Daniel Dickinson
Mlo wa dola 1.20 New York, unagharimu mkazi wa Sudan Kusini dola 349.

Mlo wa dola 1.20 New York, wamgharimu mkazi wa Sudan Kusini dola 349- WFP

Amani na Usalama

Bei ya mlo mmoja imesalia kuwa kubwa zaidi kwa wakazi walio kwenye nchi zinazokabiliwa na mizozo na vita, limesema hii shirika la mpango wa chakula duniani, WFP wakati likizindua kipimo cha bei za mlo duniani

Msemaji wa WFP huko Geneva, Uswisi, Herve Verhoosel amesema utafiti  huo ulijumuisha mataifa 52 yanayoendelea na lengo ni kuwapatia walaji katika mataifa tajiri na yenye viwanda taswira halisi ya kiwango cha fedha kinachohitajika ili mkazi wa nchi zinazoendelea aweze kuweka mlo wake mezani.

Mlo wa mkazi wa jimbo la New York, Marekani ukiwa ndio kigezo, WFP inasema mkazi wa New  York, atalipa dola 1.20 kupata mlo mmoja sawa na asilimia 0.2 ya mshahara wake kwa siku ilihali kwa Sudan Kusini italazimu mtu atumie dola milioni 348 kwa mlo huo huo.

“Mlo  huo ni supu au mchuzi ambao una maharage au kunde, mchele au nafaka yoyote pamoja na maji na mafuta,” amesema Verhoosel akisema kwa Sudan Kusini gharama hiyo inayolipwa ni sawa na asilimia 200 ya mshahara wa mtu mmoja kwa siku

Amesema “hii ina maana kwamba nchini Sudan Kusini, mchuzi tu wa kawaida unagharimu mshahara wa siku mbili, kama unfanya kazi au bahati ya kupata kazi. Takribani mara 200 zaidi kuliko tajiri za magharibi.”

Hata hivyo Bwana Verhoosel ametaja sababu nyingine za kupanda kwa bei za vyakula..

“Mabadiliko ya tabianchi, majanga huathiri bei ya vyakula, lakini utulivu wa kisiasa na kijamii ni muhimu kwa bei za vyakula kuwa nchini. Katika siku hii ya chakula duniani, nadhani hiki kipimo cha bei za vyakula kinapaswa kufungua macho yenu. Katika  nchi hizo bila miradi ya WFP na mashirika mengine, watu hao wasingaliweza kula chakula.”