Njia ya kupitisha mkataba mpya wa wahamiaji sasa ni ‘nyeupe’- UNHCR
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema sasa kuna matumaini makubwa ya kupitishwa kwa mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbiz na wahamiaji, GCM mwezi ujao.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema sasa kuna matumaini makubwa ya kupitishwa kwa mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbiz na wahamiaji, GCM mwezi ujao.
Watoto wapiganaji wa zamani katika vita vya wenye kwa wenyewe nchini Sudan Kusini , hatimaye wameaanza kuona nuru baada ya elimu inayotolewa na shirika la Veterinaires Sans Frontieres kutoka Ujerumani, kuwasaidia kujikimu. Miongoni mwa vijana hao walioachiwa huru na makundi ya wapiganaji ni James Korok mwenye umri wa miaka 19 anayeisaidia familia yake kwa shughuli ya ushonaji.
Katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja waandishi habari takriban elfu moja wameuawa wakati wanafanya kazi yao adhimu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kukomesha ukwepaji sheria kwa uhalifu dhidi ya waandishi wa habari.
Kazi ya kuhakiki wakimbizi na wasaka hifadhi nchini Uganda kwa kutumia alama za vidole na macho imekamilika kwa kubaini wakimbizi hewa 300,000 na pia kugundua kuwepo kwa wakimbizi waliotoka kambi ya Kakuma nchini Kenya. Assumpta Massoi na taarifa kamili.
Rais wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC Jaji Chile Eboe-Osuji amesema ushirikiano wa kimataifa ndio nguzo pekee ya kuendeleza kazi za mahakama hiyo iliyoanzishwa miaka 20 iliyopita.
Hivi karibuni katika mlolongo wa mijadala ya Afrika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kulifanyika mkutano wa siku moja kuhusu jinsi jamii ya kimataifa inaweza kukomesha milio ya bunduki barani Afrika, mkutano ambao ulihudhuriwa na wawakilishi wa nchi wanachama wakiwemo wabunge.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-Women, Phumzile Mlambo-Ngucka ametaka jamii ya kimataifa iachane na harakati za juujuu zisizoweza kuleta matunda katika kujumuisha wanawake kwenye ulinzi na amani duniani.
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu la UNFPA limetoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti za kukabiliana na tatizo la ghasia zilizo na uhusiano wa kingono pamoja na kijinsia nchini Sudan Kusini.
Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni maadhimisho yanayolenga kusherehekea kuanza kutumika kwa katiba ya chombo hicho tarehe 24 Oktoba mwaka 1945.
Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, kupitia timu ya kitengo cha ufuatiliaji wa wakimbizi wa ndani (DTM) leo limehitimisha zoezi la usajili wa wakimbizi wa ndani kwa kutumia alama za mwili kama vidole na macho katika baadhi ya vituo nchini Sudan Kusini.