Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi halali Uganda ni milioni 1.1; yasema UNHCR

Mtoto mkimbizi wa Sudan Kusini anachungulia akiwa kwenye lori kabla ya kusafirishwa kuelekea makazi mpya ya Imvepi wilayani Arua, kaskazini mwa Uganda UNHCR/David Azia

Wakimbizi halali Uganda ni milioni 1.1; yasema UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Kazi ya kuhakiki wakimbizi na wasaka hifadhi nchini Uganda kwa kutumia alama za vidole na macho imekamilika kwa kubaini wakimbizi hewa 300,000 na pia kugundua kuwepo kwa wakimbizi waliotoka kambi ya Kakuma nchini Kenya. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

Kazi hiyo iliendeshwa kwa pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uganda na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR kufuatia kuwepo kwa shaka na shuku juu ya idadi kamili ya wakimbizi nchini humo.

Mwakilishi wa  UNHCR nchini Uganda, Joel Boutroue amesema kazi ya uhakiki ilianza mwezi Machi mwaka huu na imekamilikia huko makazi ya wakimbizi ya Bidibidi iliyoko kaskazini mwa Uganda pamoja na wakimbizi walioko mjini Kampala.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya simu, mwakilishi huyo amesema katika uhakiki wamepata idadi ya wakimbizi kuwa ni milioni 1.1 na kwamba, "Uhakiki huu umeonyesha kupungua kwa takbani watu 300,000  tofauti na idadi tuliyokuwa nayo  mwezi Machi mwaka huu ttulipoanza  mchakato wa uhakiki."  

Mwakilishi huyo akazungumzia pia mwelekeo baada ya kukamilisha kazi hii ya utambuzi wa wakimbizi kwa kutumia alama za mwili ni ,  “Kuweka mfumo huu utumike kwa muda mrefu. Tutajadili hili kwa muda mrefu. Tunaanza mashauriano na serikali kuona kama watapenda kuendelea na mfumo huu wa uhakiki ambao tumetumia kwa wakimbizi wa kutumia alama za vidole na macho au wanataka kitu kingine, tutaona.”

Soundcloud