Kuna haja ya kujikita na waathirika wakubwa wa mzozo wa Sudan Kusini:UN/AU
Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika AU ambao uko ziarani Sudan Kusini kwa siku tatu, umeonyesha mshikamano wake na watu pamoja na uongozi wa nchi hiyo ukisema uko tayari kuunga mkono mkataba wa amani uliotiwa saini hivi karibuni mjini Addis Ababa.