Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dkt bingwa wa upasuaji Sudan Kusini ashinda tuzo ya wakimbizi 2018: UNHCR

Dkt. Atar Adaha akiwa katika chumba cha upasuaji katika hospitali ya Maban iliyoko katika kaunti ya Bunj, Sudan Kusini.
Credit English (NAMS)
Dkt. Atar Adaha akiwa katika chumba cha upasuaji katika hospitali ya Maban iliyoko katika kaunti ya Bunj, Sudan Kusini.

Dkt bingwa wa upasuaji Sudan Kusini ashinda tuzo ya wakimbizi 2018: UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Licha ya vita vinavyoendelea na changamoto nyingine lukuki nchini Sudan Kusini, Daktari mmoja bingwa wa upasuaji nchini humo amedhamiria kufanya kila awezalo kuokoa maisha ya maelfu ya wakimbizi wa ndani nchini humo,  huku akifanya kazi katika mazingira magumu yaliyomfanya kutunukiwa tuzo ya wakimbizi mwaka huu. 

Ni katika hospitali ya Maban ambayo ni hospital pekee kwenye kaunti ya Bunj Kaskazini Mashariki mwa Sudan Kusini,  Dkt. Evan Atar Adaha katika katika kibarua cha kila siku, ni mganga mkuu wa upasiaji na mkurugenzi wa hospitali hiyo , leo ametunukiwa  tuzo ya umoja wa Mataifa ya wakimbizi ijulikanayo kama tuzo ya Nansen  kama mshindi wa mwaka huu 2018. Anaeleza kwa nini hospitali yake ni muhimu sana.

“Tangu vita vilipozuka mwaka 2013 Sudan Kusini hospital nyingi katika jimbo la Upper Nile zilisambatatishwa kwa hiyo hii ndiyo hospital pekee inayofanya kazi kikamilifu katika jimbo zima , hivyo jimbo zima wanakuja hapa tunazungumzia idadi ya watu 200,000.”

Dkt. Atar Adaha akiwa na mkimbizi kutoka Sudan ambaye nasubiri kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kujifungua kwenye Hospitali ya Maban, Kaunti ya Bunj, Sudan Kusini.
UNHCR/Will Swanson
Dkt. Atar Adaha akiwa na mkimbizi kutoka Sudan ambaye nasubiri kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kujifungua kwenye Hospitali ya Maban, Kaunti ya Bunj, Sudan Kusini.

Hospitali yake inafanya operesheni 58 kwa wiki katika mazingira magumu wakikabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa , vitanda, dawa na vitu vingine vya muhimu. Hospitali hiyo inatumika kama hospitali ya wazazi, na inatibu pia magonjwa mengine ikiwemo ukimwi na kifua kikuu na inafanya kazi kwa saa 24.

Dkt. Atar anasema tuzo hiyo ni faraja kubwa na ni kama nyota ya jaha kwake , timu nzima ya wauguzi na hospital ya Maban kwani

“Tutakapopata fedha zinazoambatana na tuzo hii tutazitumia kutatua changamoto zetu , najua fedha tutakazopata huenda zisitoshe kukidhi kila tunachohitaji lakini zitasaidia kutokana na vipaumbele vyetu nini kitashughulikiwa kwanza.”

Dkt. Atar Adaha akiwa na mkimbizi kutoka Sudan aliye na mtoto wake mwenye utapiamlo. Ni katika kituo cha kuimarisha lishe cha Hospitali ya Maban kaunti ya Bunj Sudan Kusini.
Credit English (NAMS)
Dkt. Atar Adaha akiwa na mkimbizi kutoka Sudan aliye na mtoto wake mwenye utapiamlo. Ni katika kituo cha kuimarisha lishe cha Hospitali ya Maban kaunti ya Bunj Sudan Kusini.

Dkt. Atar ametunukiwa tuzo hiyo leo mjini Geneva Uswis na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kutambua na kuthaimini mchango mkubwa na kujitolea kwake kutoa huduma ya afya kwa watu zaidi ya 200,000 wakiwemo wakimbizi zaidi ya 140,000 kutoka jimbo la Blue Nile.

Lakini kwa miaka 20 Dkt. Atar amekuwa akijikita na kutopa huduma ya afya kwa maelfu ya wakimbizi waliolazimika kuhama makwao kutokana na vita na mateso nchini Sudan na Sudan Kusini.

Tweet URL