Paza sauti kutetea haki za binadamu- kilele ni leo!
Leo ni siku ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni tarehe ya kukumbuka kupitishwa kwa azimio la haki za binadamu duniani, UDHR ambalo leo linatimiza miaka 70.
Leo ni siku ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni tarehe ya kukumbuka kupitishwa kwa azimio la haki za binadamu duniani, UDHR ambalo leo linatimiza miaka 70.
Wakuu wa nchi na serikali, mawaziri, viongozi wengine wa ngazi ya juu, asasi za kiraia na wawakilishi toka sekta za umma na binafsi wamekusanyika mjini Marrakech nchini Morocco, kwa ajili ya mkutano wa ngazi ya juu kwa lengo moja tu, kupitisha mkataba wa kimataifa wa uhamiaji.
Miaka 70 tangu kupitishwa kwa mkataba wa kimataifa wa kuzuia mauaji ya kimbari, bado watu wanauawa, wanabakwa, nyumba zao kutiwa moto, wananyang’anywa ardhi zao kwa sababu tu ya utambulisho wao.
Mkutano wa mwaka wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi wa dharura kwa majanga yanayokumba binadamu, CERF umefanyika leo jijini New York, Marekani ambapo Katibu Mkuu wa umoja huo, Antonio Guterres amesema CERF amesihi wahisani kuchangia zaidi ili kufikia lengo la uchangiaji la dola bilioni 1 kwa mwaka lililowekwa na Baraza Kuu la umoja huo miaka miwili iliyopita.
Hospitali ya wakimbizi ya Maaban iliyoko jimbo la Bunj nchini Sudan Kusini iko katika shinikizo kubwa baada ya kuzidiwa na wimbi la wagonjwa huku vifaa, wauguzi na dawa vikiendelea kuwa haba.
Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, AU wametoa taarifa ya pamoja ya maelezo yao juu ya kuchukizwa na na visa vya ukatili wa kingono, ikiwemo kubakwa, vilivyotekelezwa dhidi ya wanawake na wasichana takriban 150 karibu na mji wa Bentiu nchini Sudan Kusini mwishoni mwa mwezi uliopita.
Wachunguzi wa masuala ya haki za binadamu wanamiminika huko Bentiu nchini Sudan Kusini kuchunguza madai ya visa vya kubakwa kwa wanawake na wasichana 150 kwa siku 10 mwishoni mwa mwezi uliopita.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan kusini UNMISS umelaani vikali mfululuzo wa mashambulizi ya ukatili wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana waliokuwa wakisafiri kutoka vijijini kwao kuelekea Bentiu kwenye jimbo la Unity.
Umoja wa Mataifa umesema walinda amani zaidi kutoka chombo hicho watapelekwa kwenye jimbo la Nile Magharibi huko Sudan Kusini ili kufanikisha urejeshaji wa raia waliokimbia kutokana na mapigano.
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa María Fernanda Espinosa, amesema anaelewa fika uamuzi wa baadhi ya mataifa wa kutokuwa tayari kutia saini makubaliano mapya kuhusu uhamiaji baadaye mwaka huu.