Raia wa DRC wafurumushwa Angola, UNHCR yaingiwa wasiwasi
Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR lina wasiwasi mkubwa kutokana na wimbi kubwa la idadi ya wakimbizi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wanaorejea nyumbani kufuatia hatua ya serikali ya Angola kufukuza wahamiaji.