Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dawa mpya za majaribio dhidi ya Ebola zaanza kutumika DRC

Kituo cha kutibia Ebola katika hospitali moja mjini Beni, mkoa wa kivu Kaskazini DRC
MONUSCO/Alain Coulibaly
Kituo cha kutibia Ebola katika hospitali moja mjini Beni, mkoa wa kivu Kaskazini DRC

Dawa mpya za majaribio dhidi ya Ebola zaanza kutumika DRC

Afya

 

Dawa mpya za majaribio zimeaanza kutumika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kwa mara ya kwanza kama sehemu ya tiba ya kupambana na Ebola. 

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, dawa tano za majaribio ya kutibu Ebola zilizokuwa zikifanyiwa uchunguzi, zimeidhinishwa kwa matumizi , na nne kati ya dawa hizo zimeanza kutumika Oktoba Mosi mwezi huu , tayari wagonjwa 47 wamepewa dawa hizo.

Wagonjwa sasa wanapatiwa dawa hizo saa chache tu baada ya kuthibitishwa wameambukizwa Ebola. William Fischer ni mratibu wa kudhibiti maradhi kutoka WHO

(SAUTI YA WILLIAM FISCHER)

Nadhani hili linawakilisha mabadiliko katika mtazamo wetu wa tiba dhidi ya virusoi vya Ebola. Sasa tuna fursa ya kutoa dawa hizi ambazo huenda zikafanya kazi dhidi ya virusi hivyo. Kwangu mimi hii ni hatua muhimu katika kusonga mbele kwa mantiki ya kipi tulichonacho kwa wagonjwa wenye maradhi haya.”

 Anahisi vipi kuanza kugawa dawa hizo?

(SAUTI YA WILLIAM FISCHER )

“Naweza kusema ni hisia mchanganyiko , unapokwenda kwenye kituo cha kutibu Ebola na kugawa moja ya dawa hizi. Kwa upande mmoja , kwa upande mmoja unakuwa na hofu kubwa kwa sababu sio watu wengi waliopewa dawa hizi hapo kabla na sio wengi waliokwisha pewa.Lakini kwa upande mwingine kuna shauku kubwa na matumaini , kwa sababu kwa mara ya kwanza tuna silaha ya kutumia kupambana moja kwa moja na virusi”

 Naye rais wa muungano wa kimataifa wa hatua za tiba (ALIMA) Richard Kojan anasema

Nina furaha kwamba dawa hatimaye zipo kwa ajili ya watu wa Congo , hata kwa wale wanaoishi mbali na mji mkuu, ili sisi madaktari tuweze kuzitoa kwa wagonjwa.”

 Dawa hizo zinatolewa kwa uangalifu na kwa kuzingatia mfumo maalumu ujulikanao kama “uangalizi wa matumizi ya dharura ya tiba, ambayo haijaorodheshwa na yanayochunguzwa (MEURI).

Wataalamu wa WHO wanahusika nchini DRC katika kusaidia kubaini tiba bora kwa kutegemeana na vigezo, changamoto na uwezo wa ufuatiliaji.

Pamoja na ugawaji wa dawa hizo mpya za majaribio kuna juhudi zingine zinazoendelea sambamba ili kuanzisha vituo vya majaribio kwa ajili ya tiba, haraka iwezekanavyo.