Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Burundi

Mwanamke katika shamba la nanasi akikagua nanasi nchini Zambia.
UNDP

Zambia yaendelea kuwakirimu wakimbizi licha ya changamoto za ukame na rasilimali: UNHCR

Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, ambalo limesema kwa kuzingatia sera yake jumuishi, nchi hiyo inakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. 

Sauti
2'5"
Fortuné Gaetan Zongo, Mtaalamu UN kuhusu hali ya Haki za Binadamu nchini Burundi, akihutubia kikao cha 57 cha Baraza la Haki za Binadamu UMOJA WA MATAIFA huko Geneva, Uswisi.
UN

Burundi: Hali  ya haki za binadamu inatia wasiwasi – Zongo

Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali  ya Haki za Binadamu nchini Burundi Fortuné Gaetan Zongo, amehutubia mkutano wa 57 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi hii leo na kueleza kuwa hali ya kibinadamu katika taifa hilo la Maziwa Makuu bado inatia wasiwasi kwani mazingira yaliyosababisha kuanzishwa kwa jukumu la kufuatilia hali hiyo Burundi bado yako.