Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya UN yatiwa hofu na visa vya utesaji watu Burundi, yataka serikali ichukue hatua

Waandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mateso wakihutubia waandishi wa habari. (Maktaba)
UN Photo/Rick Bajornas
Waandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mateso wakihutubia waandishi wa habari. (Maktaba)

Kamati ya UN yatiwa hofu na visa vya utesaji watu Burundi, yataka serikali ichukue hatua

Haki za binadamu

Kamati ya Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu dhidi ya Utesaji, CAT imetamatisha kikao chake cha 78 huko Geneva, Uswisi kwa kuto  hitimisho za ripoti za mataifa 6 ikiwemo Burundi ambapo inaonesha wasiwasi juu ya utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa dhidi ya Mateso na adhabu za kikatili zisizoheshimu utu.

Taarifa iliyotolewa mjini Geneva, Uswisi na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR imemnukuu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Claude Heller, akisema kamati imeshtushwa na madai ya kuaminika ya unyanyasaji, kuteswa, kunyongwa bila haki na watu kutoweshwa nchini Burundi tangu mzozo wa kisiasa wa 2015.

Halikadhalika imeshangazwa na ripoti zinazoendelea za mauaji ya kiholela yanyoripotiw kufanywa na askari wa vikosi vya usalama, vikosi vya jeshi, Ofisi ya Usalama wa Taifa, na tawi la vijana la chama tawala lijulikanalo kama Imbonerakure. 

Kamati pia imeonesha wasiwasi mkubwa juu ya madai ya mateso na utesaji unaofanywa na makundi hayo hasa katika majengo ya Huduma ya Taifa ya Ujasusi karibu na kanisa kuu la mji mkuu wa kibiashara Bujumbura, vituo vya polisi, magereza, na vituo vingine vya kushikilia watu vizuzi.

“Serikali iwe na udhibiti mkali dhidi ya polisi na vikosi vya usalama ili kuzuia mauaji ya kiholela, kuchunguza tuhuma zote za mauaji ya kiholela, kiholela na kuwafungulia mashtaka na kuwaadhibu wale waliohusika,” amesema Bi. Heller.

Kamati imeitaka serikali ya Burundi kuchunguza kila kesi ya madai ya mateso au utesaji kwa kutumia chombo kisichoegemea upande wowowte huku ikiiomba serikali ihakikishe kuwa washukiwa, ikiwa ni pamoja na wale walio katika nafasi za uongozi, wanafikishwa mahakamani ipasavyo na, ikiwa watapatikana na hatia, wapatiwe adhabu inayofaa kulingana na uzito wa kosa.

Nchi zingine zilizohushwa kwenye ripoti hiyo ni Costa Rica, Denmark, Kiribati, Misri na Slovenia.

Ripoti kamili, bonyeza hapa.