Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Hitaji la dharura kuboresha mifumo ya udhibiti wa taka laonekana baada ya taka zilizotokana na kudhibiti COVID-19 kuwa tishio

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO limetoa ripoti mpya inayoonesha kuwa mifumo ya usimamizi wa taka za afya duniani kote hivi sasa imezidiwa uwezo kutokana na maelfu ya tani za taka zinazotokana na vifaa vilivyotengenezwa kwa ajili ya kukabiliana na janga la COVID-19 na hivyo kutish

Sauti -
2'44"

Chanjo ya bilioni 1 dhidi ya Covid-19 yasambazwa kupitia COVAX

Kutokana na chanjo milioni 1.1 zilizofikishwa nchini Rwanda wikendi hii,  mpango wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa wa kuhakikisha utoaji sawa wa chanjo kwa wote umefikia hatua ya bilioni moja. 

WHO yapendekeza dawa mbili mpya za kutibu wagonjwa wa COVID-19

Kundi la wataalamu wa miongozo wa WHO wametaja dawa ya Baricitinib kwa ajili ya kutibu wagonjwa mahututi  wa COVID-19.Dawa nyingine iliyopendekezwa na wataalamu hao ni Monoclonal, na pia kutoa masharti ya matumizi ya kingamwili hiyo kutumika kwa wagonjwa walio na Covid-19 isiyo kali, lakini tu kwa wale walio katika hatari kubwa ya kulazwa hospitalini.

Omicron ilichochea wimbi la Covid-19 barani Afrika lakini inapungua haraka 

Baada ya wimbi la ugonjwa wa Covid-19 lililodumu kwa takribani wiki sita, wimbi hilo la nne barani Afrika ambalo kimsingi lilichochewa na mnyumbuliko wa virusi vya corona kwa jina Omicron, sasa linapungua na hivyo kulifanya kuwa wimbi lililodumu kwa muda mfupi zaidi katika bara hilo ambako jumla ya maambukizi hivi sasa tangu kuibuka kwa ugonjwa huo limezidi milioni 10. Imeeleza taarifa ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa kanda ya Afrika iliyotolewa hii leo Brazzaville nchini Congo.  

13 JANUARI 2022

Miongoni mwa tuliyonayo hii leo katika habari za Umoja wa Mataifa

Sauti -
12'31"

Omicron isidharauliwe na kukosa usawa wa chanjo kunatuumiza zaidi - WHO

“Kutokana na kuenea kwa mnyumbuliko mpya wa omicron katika maeneo yote duniani, maambukizi mapya yalifikia milioni 9.5 na vifo vilizidi 41,000 ulimwenguni kuanzia Desemba 27 hadi Januari 2. "Na tunajua kwamba namba hizi ziko chini ya zile halisi." Anaonya Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, Dkt Tedros Ghebreyesus akitoa wito kwa mara nyingine tena kwa usambazaji sawa wa chanjo dhidi ya virusi vya corona. 

Kampeni ya #ACTogether kutumika wakati wa Kombe la Kiarabu la FIFA

Kwa kutumia jukwaa la Kombe la kwanza la Kiarabu la FIFA™, Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, WHO, FIFA na mamlaka ya Qatar wanazindua kampeni ya #ACTogether ili kutoa wito wa ushirikiano na umoja ili kuhakikisha upatikanaji sawa wa chanjo, matibabu na vipimo vya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona, COVID-19.

WHO yatoa muongozo wa vyeti vya chanjo ya COVID-19 kielektronik

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema ingawa haliungi mkono mahitaji ya uthibitisho wa chanjo ya COVID-19 ili mtu kuweza kusafiri lakini katika mazingira mengine kulingana na tathmini ya hatari ya nchi zinazohusika, taarifa kuhusu chanjo dhidi ya COVID-19 zinaweza kutumika

Sauti -
1'43"

Kuelekea kuhifadhi taarifa za chanjo ya Covid-19 kidijitali, WHO yatoa mwongozo

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema ingawa haliungi mkono mahitaji ya uthibitisho wa chanjo ya COVID-19 ili mtu kuweza kusafiri lakini katika mazingira mengine kulingana na tathmini ya hatari ya nchi zinazohusika, taarifa kuhusu chanjo dhidi ya COVID-19 zinaweza kutumika kupunguza mahitaji ya karantini au upimaji wakati wa kuwasili katika nchi hizo.

Mtanzania atengeneza mashine ya Oksijeni ambayo haina ulazima kuwa na mtungi wa gesi

George Nyahende, raia wa Tanzania amebuni na kutengeneza mashine ya oksijeni ambayo ina sifa za kipekee ambazo anasema zinatokana na mazingira hususani ya vijiji vya Tanzania.