Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Dorica Zuze na mwanae akiwa katika kituo cha afya  nchini Malawi.
© UNFPA/Joseph Scott

Tusijidanganye, wimbi la tatu la Covid-19 Afrika halijaisha kabisa - WHO

Baada ya wiki nane mfululizo za kuongezeka kwa kasi ya maambukizi, sasa maambukizi mapya ya  Covid-19 barani Afrika yamepungua kasi, Afrika Kusini ambayo ndiyo ilikuwa na idadi kubwa ya maambukizi ikishuhudia kushuka kwa kasi kwa maambukizi mapya ingawa maendeleo haya yanaweza kuwa ya muda mfupi, takwimu mpya kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO zimeonesha.