Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanjo ya bilioni 1 dhidi ya Covid-19 yasambazwa kupitia COVAX

Chanzo zilizotolewa kwa Tanzania kwa msaada wa Marekani kupitia mpango wa Umoja wa Mataifa wa kusaka chanjo za Corona au COVID-19, COVAX, na ziliwasili tarehe 24 Julai 2021.
UNICEF/Daniel Msirikale
Chanzo zilizotolewa kwa Tanzania kwa msaada wa Marekani kupitia mpango wa Umoja wa Mataifa wa kusaka chanjo za Corona au COVID-19, COVAX, na ziliwasili tarehe 24 Julai 2021.

Chanjo ya bilioni 1 dhidi ya Covid-19 yasambazwa kupitia COVAX

Afya

Kutokana na chanjo milioni 1.1 zilizofikishwa nchini Rwanda wikendi hii,  mpango wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa wa kuhakikisha utoaji sawa wa chanjo kwa wote umefikia hatua ya bilioni moja. 

Kwa kushirikiana na Ushirika wa ubunifu wa maandalizi dhidi ya milipuko ya magonjwa ,CEPI, Muungano wa Chanjo GAVI, na wadau wengine, WHO imeongoza operesheni kuwa zaidi ya ununuzi na usambazaji wa chanjo katika historia kwa kufikisha chanjo katika nchi 144 hadi kufikia sasa.  

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Jumapili hii, kufikia tarehe 13 Januari 2022, kati ya nchi 194 wanachama wa WHO, 36 wamechanja chini ya asilimia 10 ya watu wao, na nchi 88 chini ya asilimia 40. 

"Matamanio ya COVAX yaliathiriwa na kujilimbikizia katika nchi tajiri, milipuko ya janga iliyosababisha mipaka na usambazaji kufungwa na ukosefu wa kupeana leseni, teknolojia, na ujuzi wa makampuni ya dawa ulisababisha uwezo wa utengenezaji kutotumika.” WHO imeeleza. 

Mnamo tarehe 24 Februari 2021, Ghana ilikuwa nchi ya kwanza duniani kupokea chanjo kupitia COVAX wakati dozi 600,000 za chanjo ya Oxford–AstraZeneca ziliwasilishwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Accra. 

Kazi iliyobaki 

COVAX kwa sasa inafanya kazi na serikali, watengenezaji na washirika wake ili kuhakikisha kuwa nchi zinapopokea chanjo, zinaweza kuwafikishia watu haraka. 

"Kazi ambayo imeingia katika hatua hii (bilioni 1) ni ukumbusho tu wa kazi iliyosalia", shirika la afya la Umoja wa Mataifa limesisitiza likiongeza kuwa huku kukiwa na chanjo zilizoko njiani, wananchi wanapaswa kudai kwamba serikali na kampuni za dawa zigawane zana za kiafya kimataifa na "kukomesha mzunguko wa vifo na uharibifu wa janga hili, kupunguza minyumbuliko mipya na kuinua uchumi wa dunia".